Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa ilikuwa katika Kikao Kisiwandui, Zanzibar, kwenye ishu kubwa zilizojadiliwa zipo zinazohusu sakata la Escrow na pia ishu ya waliopewa adhabu kwa kukiuka maadili ya chama kwenye mchakato wa kugombea Urais 2015.
Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye alitoa taarifa kuhusiana na maazimio ya CCM kuhusu ishu hizo; “Kamati
kuu inaitaka Serikali na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza
maazimio ya Bunge yaliyobaki, pili kamati kuu imewataka wale wote
waliopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao na
wasipowajibika, waliowapa dhamana wachukue hatua ya kuwawajibisha.
Kwamba
kutokana na sakata hili na jinsi lilivyokwenda Kamati Kuu inataka
wanopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika inapotakiwa kuwajibika
na wasipowajibika wao wale waliowapa dhamana wachukue hatua za
kuwawajibisha“
“Kamati
Kuu imeiagiza Kamati ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa
wale wote waliohusika na ukiukwaji wa maadili katika sakata la Escrow,
ambao wako kwenye vikao vya maamuzi vya chama katika sakata hili wako
viongozi wetu wa chama, ambao wapo kwenye vikao vya maamuzi kwa maana ya
Kamati Kuu na Halmashauri Kuu na kwa namna moja ama nyingine
wamehusishwa kwenye sakata hili na vitendo vyao vimehusishwa na
ukiukwaji wa maadili“– Nape Nnauye.
Makada
6 wa CCM waliopewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye
mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea Urais, watamaliza muda wa
adhabu zao Mwezi wa pili mwaka huu 2015… itafanyika tathimini kuona kama
walizingatia masharti ya adhabu zao na kama kuna ambao watakutwa
hawakuzingatia masharti ya adhabu zao au wamefanya matendo ya ukiukwaji
tena wa maadili wataongezewa adhabu“– Nape Nnauye.
Nape aliwatangaza waliopewa onyo hilo kuwa ni Edward Lowassa, Frederick Sumaye, January Makamba, Steven Wassira, Benard Membe na William Ngeleja.
No comments:
Post a Comment