Hizi ni moja ya story ambazo hatujazoea kuzisikia kwa watu kama wa Bongo, eti kutoa dola 400 kumtibia samaki?
Kutoka Norfolk Uingereza, jamaa mmoja ametumia dola 465 kumtibu samaki wake aina ya Goldfish aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la tumbo ambapo alikuwa na tatizo katika mfumo wa kuyeyusha chakula.
Aligundua kwamba hali ya samaki wake sio
nzuri, hakujua ukubwa wa tatizo, ila alipofika kwa mtaalamu wa masuala
ya wanyama aliambiwa kinachotakiwa kufanyika, operation ambayo ikachukua
kama dakika hamsini hivi.
Daktari Faye Bethell ndiye aliyesimamia zoezi hilo la upasuaji na baadaye samaki huyo akashonwa nyuzi tatu.
No comments:
Post a Comment