Pages

January 20, 2015

MKUTANO MKUU WA BARAZA LA WATOTO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAANZA LEO MJINI DODOMA

Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni chombo cha kuwashirikisha watoto katika maamuzi mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Baraza la Watoto lilianzishwa mwaka 2002 likiwa na lengo la kuongeza ushiriki wa watoto katika ngazi mbalimbali za jamii kama  mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (CRC) ulivyoeleza ambapo Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa mataifa unapaswa kuutekeleza.

kila baada ya miaka 2 Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hufanya mabadiliko ya uongozi katika kuliendesha Baraza la watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia na mwaka huu uchaguzi utafanyika tarehe 21 Januari 2015 baada ya ule wa mwaka 2013.

Wizara Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto hufanya uratibu na kusimamia uanzishwaji na uendeleshaji wa Baraza hili na mengine yaliyopo katika mikoa yetu.

serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kuboresha ushiriki huo wa mtoto kwa kuchukua hatua mbalimbali kama ifuatavyo.

·         Kuandaa katiba ya Baraza la  Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
·         Kuandaa mwongozo wa uundwaji wa mabaraza ya watoto katika ngazi za Taifa,mikoa,wilaya,kata na vijiji/mitaa.

·         Kuandaa na kusambaza kielekezi cha ushiriki wa mtoto
·         Kuandaa mpango kazi wa Taifa wa ushiriki wa mtoto
·    Kuwashirikisha watoto katika maamuzi mbalimbali ya kitaifa na kimataifa – km kutoa maoni katika utengenezaji wa katiba mpya ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maandalizi ya sera ya mtoto ya afrika mashariki ambapo wawakilishi wa watoto nchini walishiriki.
Watoto kutoka mikoa Mbalimbali ya Tanzania katika picha ya pamoja na Paul Ngusa (katikati)Msaidizi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ummy Jamaly (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rauhiya Ameir (wa kwanza kulia) Makamu Mwenyekiti, Jaqueline Namfua (wa pili kushoto) Afisa Habari UNICEF, Christopher Mushi (wa kwanza kushoto) Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Wizara Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...