Katibu
wa Kamati ya Tathmini wa Taasisi ya Ushauri wa Biashara, Ernest
Mwamwaja (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni zinazowajibika kwa jamii kutambuliwa
Machi mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa
Shughuli za Maendeleo ya Jamii, Abraham Shempemba na Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Ushauri wa Biashara, Dickson Hyera.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
mbali mbali zinazotoa huduma kwa jamii zinatarajiwa kutambuliwa na
kutolewa tathimini ya uwajibikaji wake machi mwaka huu.
Akizungumza
Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa Ushauri wa
Biashara, Dickson Hyera alisema lengo ni kurudisha sehemu ya biashara
kwa jamii kama sehemu ya shukrani.
Alisema
pia italeta faida nyingine ikiwa ni pamoja na kuleta mahusiano mazuri
na kampuni nyingine ambapo matoko yatakayotoka yataleta hamasa kwa
kampuni nyingine kurudisha sehemu yao ya biashara katika jamii.
Hyera
alisema tafiti zinaonesha kuwa kampuni za nje ndo zinahusika zaidi
katika jamii hususani katika masuala ya elimu, mindombinu, maji na
huduma nyingine za kijamii.
"Tayari
kunataasisi nyingine zimeshafanya marejesho hayo na nyingine hazijaleta
hivyo nyingine zijitokeze kuonesha nia ya kushiriki ili ziweze
kunufaisha jamii," alisema.
Aliongeza
kuwa mchakato huo pia unalenga kutathimini kwa kulinganisha takwimu za
mirejesho ambayo inafanywa na taasisi kuthaminisha na kung'amua kuhusu
manufaa hayo na gharama zake.
Alisema
madhumuni makubwa ya tathmini hiyo yanajumuisha kuona jinsi gani
taasisi mbalimbali zinazojitoa kwaajili ya kusaidia jamii, kutambua na
kuthamini wanaofanya vizuri, jinsi taasisi hizo zinavyochangia kufanya
maisha ya wanajamii kuwa bora kwa kuzingatia idadi ya misaada ambayo
inatolewa na thamani zake.
Naye
Katibu wa Kamati ya Tathmini Ernest Mamwaja alisema kuna watu
wananufaika lakini hawajui wamesaidiwa na nani hivyo watajua, pia
wanaotoa msaada wanaweza kuleta nguvu katika maeneo ambayo manufaa yake
ni makubwa.
Alisema
tafiti ambazo zimeonesha kuwa kampuni ambazo zinarejesha kwa jamii
zinamanufaa makubwa ikiwa ni pamoja na soko kupanda, hivyo lengo si
kuangalia nani mshindi au nani amefanyanini ali ni kwaajili ya manufaa
ya watanzania.
No comments:
Post a Comment