Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,
akisalimiana na wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuaza mchezo wa Nusu
Fainali ya pili kati ya Simba na Polisi uliofanyika katika uwanja wa
Amaan, Simba imeshinda bao 1--0, Itacheza fainali na timu ya Mtibwa
baada ya kuitowa timu ya JKU kwa penenti 4--3.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,
akiwasalimia wachezaji wa timu ya Polisi kabla kuaza kwa mchezo wao na
timu ya Simba.mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan
Kikosi cha timu ya Simba kilichoilaza timu ya JKU katika mchezo wa Nusu Fainal, uliofanyika uwanja wa Amaan.
Wachezaji wa Timu ya Polisi OLIwakiomba dua kabla ya mchezo wao kuaza wa
Nusu Fainal uliofanyika uwanja wa Amaan, Timu ya Simba imeshinda bao
1--0.
Kikosi cha timu ya Polisi kilichopambana na timu ya Simba katika mchezo wa Nusu Fainali uliofanyika uwanja wa Amaan
Dk.Shein:Tofauti za Kisiasa na Vyama Zisitufanye Kukiuka Taratibu na Sheria za Kuendesha Shughuli za Kisiasa.
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 11 Januari, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesisitiza tena umuhimu wa viongozi wa kisiasa kufuata sheria na
taratibu zilizowekwa katika kuendesha shughuli zao za kisiasa na kuwa
tofauti za vyama isiwe sababu ya viongozi hao kukiuka utaratibu na
sheria hizo.
Akizungumza
mara baada ya kupokea matembezi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) katika viwanja vya Mnanzi Mmoja mjini Unguja jana ikiwa ni
sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Dk. Shein
alisema kuwa “tofauti za kisiasa na vyama zisitufanye tukakiuka
utaratibu wa kisheria uliowekwa”
Alibainisha
kuwa Zanzibar inaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia kwa kufuata
Katiba na sheria zilizopo huku kukiwa na vyombo vya kusimamia sheria na
utoaji haki kwa kila mwananchi.
Dk.
Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwakumbusha
wanasiasa kutumia mfumo uliopo wa vyama vya vingi kushindana kwa sera na
hoja na kuepuka maneno ya kuwatisha wananchi na kuwatia hofu.
Alibainisha
kuwa kumekuwepo na ushirikiano mzuri katika uendeshaji wa Serikali
iliyo chini ya mfumo wa Umoja wa Kitaifa hivyo kuhoji kulikoni baadhi ya
viongozi wakiwa nje ya serikali wanafanya mambo tofauti.
“Tumekuwa
tukishirikiana vyema katika serikali kulikoni huko? Kwa nini baadhi
wanasahau utamaduni wa uongozi, lugha za viongozi na wajibu wao katika
jamii”alihoji Dk. Shein.
No comments:
Post a Comment