Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA)Dan Kigega akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Arusha.
Na Filbert Rweyemamu
Arusha.Bunge
la Afrika Mashariki limeagiza kuzingatia sheria za kifedha na
kanuni zake ili kuachana na matumizi
yasiyo ya lazima ya rasilimali kuwa ni maeneo muhimu ambayo Bunge linataka
Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) kushughulikia.
Wakati huo huo, Kamati ya Hesabu inapendekeza Baraza la Mawaziri la EAC kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha shughuli za kawaida za mihimili ya EAC na taasisi zake. Taarifa hiyo imejumuisha maudhui ya Ripoti ya mapitio ya taarifa EAC ya fedha kwa mwaka uliomalizika Juni 30 mwaka 2013.
Ripoti hiyo iliwasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za bunge hilo kwenye kikao kilichofanyika alhamisi,Jeremie Ngendakumana ambayo inatarajiwa kujadiliwa wiki hii jijini hapa.
Ilielezwa kuwa katika kuimarisha taarifa za kifedha za mihimili ya EAC,Ripoti ilionyesha kuwa kulikuwa na matumizi ya juu yaliyovuka bajeti iliyotengwa na kuliagiza Baraza la Mawaziri kuielekeza Menejimenti ya EAC kufuata sheria za fedha na kanuni zake kupata kibali kwa mamlaka husika ya matumizi ya ziada.
Pia iliitaka menejimenti kuhakikisha inaziba mianya ya kuruhusu matumizi ya masurufu yasiyofata uwajibikaji.
Ripoti ilibaini kuwa ndani ya kitengo cha ukaguzi wa ndani wa EAC kutokuwa na weredi wa kutosha wa kufanya mipango yake na mapitio husika. Hivyo kutaka kuziba mianya hiyo ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi wenye ujuzi katika uboreshaji wa mifumo ya udhibiti wa ndani ili kuimarisha usalama wa rasilimali.
Kamati hiyo pia iliona ucheleweshaji usiokuwa wa lazima katika ukamilishaji wa mapitio ya taasisi na kuonyesha wasiwasi wake kuhusu gharama kubwa za uendeshaji wa Jumuiya hiyo.
"EAC ina nafasi kadhaa za wafanyakazi ambazo hawajaajiriwa na zilizoachwa wazi,mara nyingi menejimenti imekuwa ikilazimishwa kutoa mikataba ya muda mfupi mfupi ambayo ina athari mbaya kwa wafanyakazi wenyewe na EAC kwa ujumla,"ilisema taarifa hiyo
Kamati ilipendekeza kujaza nafasi mbalimbali zilizo wazi ili kuiwezesha Jumuiya hiyo kufanya kazi zake ipasavyo na kufikia malengo tarajiwa na kufuata utaratibu sahihi wa kuajiri badala ya kutoa ajira hizo kwa wafanyakazi ambao wamekua wakipata mikataba ya muda mfupi kila mara.
Katika hatua nyingine Kamati ilibaini ili kukabiliana na matumizi yasiyokuwa ya lazima EAC iweke utaratibu wa kikomo cha juu cha siku ambazo mtumishi wake anapaswa kuwa safarini kikazi na iwapo atazidisha zinatakiwa ziwepo sababu zisizoepukika.
Kamati hiyo inayoongozwa na Ngendakumana iliiagiza Sekretarieti kushughulikia makosa katika manunuzi ya tiketi kwa ajili ya Sekretarieti ambayo yamegharimu zaidi ya dola 3.4 milioni. Sehemu ya changamoto alibainisha kuwa ni ukosefu wa idhini na hakuna njia ya wazi ya mtiririko wa taarifa ya baadhi ya matukio.
Wakati huohuo Kamati ya Hesabu ilibaini matumizi mabaya ya fedha ya Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EACJ),ikitoa mfano wa mkutano uliofanyika nje ya ofisi kutathmini zabuni na mapitio ya Mpango Mkakati ambayo ilitumia jumla ya dola za kimarekani 116,000 zililipwa kama posho za kujikimu.
Hata hivyo awali ilitarajiwa shughuli hiyo ingeweza kufanyika katika eneo mbadala ambalo kusingehitajika malipo ya kujikimu.
Kamati hiyo inapendekeza Bunge kuwaomba Baraza la Mawaziri kuelekeza Menejimenti ya EAC kufanya marekebisho ya sheria za fedha kwa wafanyakazi kwa lengo la kukatisha tamaa mikutano kufanyika mjini Moshi na kuweka kifungu cha kuhalalisha mikutano hiyo na malipo.
Pia Kamati ilitaka masuala ya wafanyakazi katika Mahakama kushughulikiwa ikiwa ni pamoja kujazwa nafasi zilizo wazi kwa kipindi cha miaka.
Kwa upande wa matumizi ya Bunge la Afrika Mashariki(EALA),Kamati ilibaini malipo yasiyo ya kawaida ya kujikimu ya kiasi cha dola 9,084 ili kuwezesha mahudhurio ya kamati ya mazishi na inapendekeza kwamba Baraza la Mawaziri litoe mwongozo kwa menejimenti ya kuandaa miongozo juu ya matumizi ya yanayohusu matumizi ya taasisi zote za EAC .

No comments:
Post a Comment