Pages

January 26, 2015

Hekaheka ya leo Jan 26 imetokea Mbezi Dar inahusu mtoto aliyetelekezwa na mama yake.



gea
Kwenye Hekaheka ya leo January 26, inaotokea Mbezi Dar inahusu mtoto anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi mitatu kutelekezwa na mama yake  kwenye nyumba ambayo haijamaliziwa kujengwa akiwa ameachwa na vitu mbalimbali.
Majirani wamesema walisikia mtoto huyo akilia walipoingia walikuta ameachwa na vitu mbalimbali likiwemo begi lenye nguo, sabuni na mafuta ndipo walipoamua kumchukua na kumpeleka kwa Mjumbe wa Serikali za mitaa na baadae waliamua kutoa taarifa kwa wananchi ili kuweza kumtambua mtoto huyo bila mafanikio, baadaye mtangazaji  wa Clouds FM, Dina Marios anaeishi eneo hilo alijitolea kuishi nae hadi mzazi wake atakapo patikana.
Wakiendelea kumtafuta mama huyo walifanikiwa kumpata ndugu wa mama mwenye mtoto ambae amesema muda mchache kabla ya tukio hilo alienda nyumbani kwake akitaka kumuachia mtoto huyo na alipomkatalia aliamua kuondoka nae, walipompigia simu mama huyo alikataa kuwa yeye sio mama wa mtoto huyo na aliposikia sauti ya ndugu yake aliamua kukata simu, mtoto huyo amechukuliwa na ndugu huyo chini ya uangalizi wa Serikali za mtaa.
gea 55
gea 55mmm

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...