Kanisa
Polisi nchini Kenya wanasema afisa mmoja wa kanisa amepigwa risasi na kuuawa alipokuwa akielekea katika maombi.
Madhumuni ya mauaji hayo hayajatambulika, lakini Muungano wa Makanisa mjini Mombasa tayari umesema ni mauji ya kidini.
Mauaji ya
afisa wa kanisa jijini Mombasa yanatishia kuhangaisha wakaazi walioanza
mwaka kwa amani baada ya machafuko mengi ya mwaka 2014.
Polisi
wanasema afisa wa kanisa moja jijini Mombasa alipigwa risasi na kufariki
alipokuwa akiingia ndani ya shule moja ambayo wameikodisha kufanya
maombi yao.Polisi Mombasa
Mkuu wa
Upelelezi wa Uhalifu Mombasa Ondiek amesema mtu mmoja aliyekuwa na
bunduki alimfuata jamaa huyo hadi akaingia ndani ya uwanja wa shule
kabla ya kumpiga risasi. Alikufa papo hapo.
Aidha
Ondiek amesema Polisi waliokuwa wameshika doria shuleni walisikia sauti
za risasi na hivyobasi kumkabili muuaji huyo, lakini akahepa ndani ya
vitongoji vilivyo karibu na shule
No comments:
Post a Comment