Maandamano ya umoja nchini Ufaransa yaanza
Maandamano
ya umoja nchini Ufaransa yameanza baada ya makundi ya watu kukongamana
katika eneo la de la Republique katika mji mkuu wa Paris nchini Ufaransa
,kama kigezo cha kuonyesha umoja dhidi ya mashambulizi ya wiki iliopita
yaliotekelezwa na waislamu wenye itikadi kali.
Zaidi ya watu millioni moja wanashiriki katika maandamano hayo.
Makumi ya
viongozi wa nchi tofauti duniani wako mji paris ambapo usalama
umeimarishwa huku maafisa zaidi wa jeshi na wale wa polisi wakiwekwa
kupiga doria.
Ghasia hizo nchini Ufaransa zilianza siku ya jumatano kutokana na shambulizi la gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Hatahivyo maafisa wa polisi waliwazingira na kuwapiga risasi mandugu wawili waliohusika na shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment