Tuzo ya Msanii DIamond Platnumz aliyoshinda Nchini Nigeria Usiku wa Leo tarehe 12 Dec 2014.
Msanii wa
Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Abdul Nassib almaarufu kama
Diamond Platnumz Anyakua tuzo nyingine ya The Future Awards zilizokuwa
zikifanyika leo usiku huko Lagos Nigeria kwa Kina Msanii Davido
Ikiwa
usiku huo huo ambao Mshiriki wa Tanzania katika Big Brother Africa Idris
Sultan anatangazwa Mshindi Na Huko Lagos Nigeria Diamond Platnumz naye
akatangazwa mshindi wa Tuzo hizo za Te Future Award 2014.
Mara
baada ya Mshiriki wa Tanzania Katika Shindano la Big Brother Africa 2014
Idris Sultan kutangazwa MShindi watanzania wengi walionekana
kufurahishwa sana na Ushindi wake huku wengine Wakimpongeza kupitia
ukurasa wao wa Tweeter muda mfupi baadae Msanii Kutoka Nchini Nigeria
Davido alionekana waziwazi kukerwa na Ushindi huu wa Mtanzania Idris na
kuamua kutweet "N They Cheat Again lol". Tweet hii imemfanya Msanii huyo
wa NIgeria kushambuliwa na Maneno na watanzania wengi katika kurasa zao
za tweeter.
Mara
baada ya Kutweet "N They Cheat Again Lol" tweet hiyo imesomeka pia Mara
baada ya Kuibuka tena Mshindi katika Tuzo Hizo za The Future Awards 2014
zilizokuwa zikifanyika Jijini Lagos Nchini Nigeria ambapo ni nyumbani
kwa Msanii Davido.
Usiku wa
leo Utakumbukwa sana na Watanzania kutokana na Kuwa Usiku mzuri kwa
Watanzania na Tanzania Kwa Ujumla kwa maana ni usiku ambao Mshiriki
kutoka Tanzania ambae alikuwa akishiriki Shindano la Big Brother Africa
Idris Sultan kutangazwa Mshindi wa Shindano hilo kwa Mwaka 2014 na
kuondoka na kitita cha Dola za Kimarekani laki tatu usiku huo huo na
Diamond Platnumz kutangazwa Mshindi wa Tuzo ya The Future awards 2014
Hongereni
watanzani kwa kutufanya kumaliza Mwaka 2014 vizuri huku Davido
akionyesha chuki zake binafsi dhidi ya watanzania na Tanzania Kwa Ujumla
No comments:
Post a Comment