Balozi
wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na wageni
waalikwa wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kwenye hafla maalum ya kuwakaribisha
na kuwapongeza wanajeshi wa kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya
Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi
kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta
chini ya kamanda Peter Christian Semrau (kulia) iliyofanyika ndani ya
meli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
KAMANDA
wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika
ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa
linaloendesha operesheni Atalanta, Peter Christian Semrau, amesema
jumuiya ya kimataifa imepata mafanikio makubwa kwa kuwezesha njia
inayotumika sana na meli kuwa salama.
Akizungumza
katika mahojiano ndani ya meli hiyo ambayo imetia nanga katika bandari
ya Dar es Salaam, Kamanda Semrau alisema kwamba kwa mwaka huu
hapakuwepo na tukio kubwa ambalo limetikisa eneo hilo la Pwani ya Pembe
ya Afrika inayopakana na Somalia na Yemen.
Alisema
kuanzia shughuli za kimataifa kukabili uharamia na ujambazi baharini
kuanza mwaka 2009 kumekuwepo na ushindi wa kimataifa kutokana na
kuendelea kupungua kwa matukio katika eneo hilo ambapo awali ilikuwa ni
tishio kubwa.
Alisema
pamoja na kupungua kwa matukio ya kijambazi na utekaji nyara kazi
ambayo inatarajiwa kufanywa mwakani ni kuhakikisha kwamba mataifa
yanayopakana na bahari ya Hindi yanawezeshwa kujilinda yenyewe dhidi ya
matukio ya baharini.
Pichani
juu na chini baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania na mabalozi
mbalimbali waliojumuika kwenye hafla hiyo wakisiliza risala ya Balozi wa
Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke (hayupo pichani).
Meli
hiyo ambayo inafanya doria kuanzia kaskazini mwa Afrika hadi Kusini
imetia nanga Dar es salaam ikitokea Madagascar ambako nako ilipata
mapokezi makubwa.
Operesheni
Atalanta inaendeshwa na vikosi vya Umoja wa Ulaya vikilinda eneo la
bahari ambalo lina shughuli nzito kwa meli za biashara
Meli hiyo ambayo itakuwa katika operesheni hadi februari mwakani itapokewa kazi hiyo na meli nyingine ya FGS Bayern.
Naye
Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke akizungumza na waandishi
wa habari akiwakaribisha katika melivita hiyo alisema kwamba
amefurahishwa na mchango wa taifa lake katika kuhakikisha pwani ya
Bahari ya Hindi upande wa Afrika inakua salama na watu wanapata huduma
zinazotakiwa.
Alisema
moja ya kazi kubwa ya meli hiyo ni kusindikiza meli zenye vyakula au
huduma mbalimbali za kijamii kwa mataifa ambayo yanashida ili kupunguza
maumivu.
Alisema
pamoja na meli hiyo kutia nanga Dar es Salaam kuonesha ushirikiano wa
kutosha kati ya taifa lake na Tanzania, anatarajia mwakani mahusiano ya
Tanzania na Ujerumani yatazidi kuimarika hasa katika nyanza za hifadhi
na maendeleo ya jamii.
Aidha
balozi huyo alisema kwamba taifa lake linaongeza fedha zaidi kwa ajili
ya uanzishaji wa mamlaka ya wanyamapori nchini Tanzania kwa lengo la
kuifanya iwe na nguvu na uwezo wa kulinda wanyama hao.
Pia
alisema inafikiria namna ya kufanya na meli ya MV Liemba ambayo alisema
ni moja ya vielelezo hai vilivyopo vyenye maana kubwa katika uhusiano
wa Tanzania na Ujerumani.
Alisema meli hiyo inafaa kufanyiwa ukarabati ili kuweza kutoa huduma kandoni mwa ziwa Tanganyika.
Aidha
alisifu ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania hasa kwa kuzingatia uhuru
uliopo wa vyombo vya habari na majadiliano yenye afya bungeni yenye
lengo la kujenga taifa lenye nguvu.
Aidha
alisema Ujerumani itaendelea kukuza uhusiano na Tanzania ambayo ni
nanga ya usalama kwa mataifa ya Afrika Mashariki na ukanda wa Bahari ya
Hindi kwa upande wa Afrika.
Balozi
wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke akifanya cheers na
mmoja wa makamanda wa jeshi la wanamaji kwenye hafla hiyo fupi
iliyofanyika ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck inayofanya
doria ya kubaini maharamia kwenye pwani ya ukanda wa Bahari ya Hindi.
Baadhi
ya wanajeshi wa kikosi cha maji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS
Lübeck kwenye hafla maalum ya kuwapongeza na kuwakaribisha nchini
Tanzania iliyoandaliwa na ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania.
Balozi
wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu (kushoto) akibadilishana
mawazo na mmoja wa maafisa wa bandari ya Dar es Salaam.
Sehemu
ya muonekano wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck wakati hafla
ya kuupongeza msafara wa kikosi cha wanamaji wa jeshi la Ujerumani
kilichoongozwa na Kamanda Peter Christian Semrau.
Baadhi ya makanda wa kikosi cha wanamaji wa jeshi hilo wakilinda lango kuu la kuingia ndani ya meli hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (kushoto)
akibadilishana mawazo na mmoja wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya
ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akihoji jambo
kwa mmoja wa wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS
Lübeck ambaye jina lake halikuweza kufahamika kiurahisi.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
Kamanda
Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya
kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari
ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni
Atalanta akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.
Wageni
waalikwa wakiendelea kupata picha ya kumbukumbu na Kamanda Peter
Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya
Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi
kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta
kubabili maharamia.
Balozi
wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke katika picha ya pamoja
na Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi huo, John Meirikion.
Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakipata picha ya pamoja ndani ya meli hiyo ya kivita.
Afisa
wa kitengo cha habari Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, John
Meirikion akipata picha ya pamoja na mmoja wa wageni waalikwa ndani ya
meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga bandari ya Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment