Pages

December 21, 2014

MHE.RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA KUTUNIKIWA KAMISHENI

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa Mstaafu Mhe Edward Lowassa walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha jana. 
Picha ya pamoja
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa akiongea na maofisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwemo na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange (kushoto) kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa alipowasili kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli
Maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu wakila kiapo cha utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete baada ya kutunukiwa kamisheni katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa kwenye sherehe hizo
Burudani katika sherehe hizo
Maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu wakitembea kwa ukakamavu walipokuwa wakitoa heshima kwa Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa hao, Monduli, mkoani Arusha
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda
Wimbo wa Taifa ulipopigwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...