Pages

December 21, 2014

MGOMBEA WA CCM ATANGAZWA MSHINDI KABLA YA KURA KUHESABIWA, CHADEMA WACHACHAMAA NA VURUGU JUU MWANZA.


Mwanza. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakazi wa Mtaa wa Ibungilo B, Kata ya Ibungilo, Wilaya ya Ilemela mkoani hapa, wamekumbwa na hali ya sintofahamu wakati wakijianda kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, baada mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM kutangazwa mshindi kabla ya wao kupiga kura.

Hali hiyo lisibabisha wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao walifurika kwenye kituo cha kupigia kura kilichopo Mtaa huo, kupinga matokeo hayo kwa madai kuwa hawajapiga kura iweje matokeo yatangazwe.

Hatua hiyo ilisababisha Polisi kuingilia kati kuwatawanya wafuasi hao kwa kupiga mabomu ya machozi, jambo ambalo lilisababisha wafusi hao kutawanyika sambamba na wananchi waliyojitokeza kupiga kura.

Wakati hayo yakitokea Mbunge wa Ilemela, Highnes Kiwia alimsimika mgombea wa Chadema, Ramadhani Saidi kuwa Mwenyekiti wa Mtaaa huo, kwa madai kwamba ndiye chaguo la wakazi wa Mtaa huo na kwamba hawawezi kuchagulia kiongozi wasiyomtaka.

Kiwia alisema, “Haiwezekani watu wamejitokeza kupiga kura, wanakuta matokeo tayari yamebandikwa, ni jambo la ajabu na lakushangaza watu hawajapiga kura matokeo yanapatikanaje, lazima suala hilo litolewe ufafanuzi wa kina.”

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimtafuta msimamizi wa uchaguzi huo Wilaya ya Ilemela ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wilaya hiyo, Justin Lukaza, na kueleza kwamba matokeo hayo ni sahihi, kwani uchaguzi wa Disemba 14 walishindwa kutangaza matokeo kutokana na tofauti zilizotokea, hivyo leo wameamua kuyatoa.

Akizungumza na mwandishi wa gazeiti hili Katibu wa Chadema tawi la Ibungilo B, Abedi Bulashi alisema kuwa uchaguzi ulifanyika Disemba 14, ulimalizika usiku wa manane, lakini kulitokea kasoro na msimamizi wa uchaguzi huo aliharisha uchaguzi na kupanga kurudiwa leo (jana).

Mmmo ya wananchi yao Daniel Buzuka alisema, “Mimi nilifika asubuhi hapa kituoni kupiga kura, lakini nilishangaa kuona polisi wanakuja na kusema hakuna uchaguzi, huu ni ubabe umetumika na wametunyima haki yetu ya masingi.MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...