Pages

November 28, 2014

IVO MAPUNDA WA SIMBA AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

Pole kipa; Ivo Mapunda amefiwa na mama yake mzazi jana usiku
Kipa huyo nambari moja wa Wekundu wa Msimbazi, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mama huyo amefia wilayani Tukuyu mjini Mbeya usiku wa jana akiwa ana umri wa miaka 75.
“Mama amefariki jana, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na hivi nipo Mbeya kwa taratibu za mazishi,”amesema Ivo.
Kifo cha mama yake huyo, kinamfanya Ivo sasa awe amepoteza wazazi wake wote wawili, kufuatia kifo cha baba yake, Philip Mapunda Februari mwaka huu, aliyefia pia Tukuyu Mbeya.
Mzee Mapunda aliyekuwa ana umri wa miaka 86 alifariki akiwa katika hospitali ya Ikonda, iliyopo Njombe ambako alikuwa amelazwa kwa takriban miezi miwili na nusu kwa maradhi ya kibofu cha mkojo, sukari na vidonda vya tumbo.  Pole Ivo na familia yake. Mungu ampumzishe kwa amani Bi Igasia Nchimbi. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...