Baadhi ya
watu wakishuhudia ajali ya basi aina ya Costal lenye namba za usajili
T410 BJD lililokuwa likifanya safari zake kati ya Tanga na Lushoto
likiwa limepinduka baada ya kugongana na Scania lenye namba namba T645
ABJ katika kijiji cha Mkanyageni wilayani Muheza. (picha: Elizabeth
Kilindi via Habari Mseto blog)
WATU 12 wamekufa papo hapo na wengine 19
wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la
abiria aina ya Toyota Costa inayosafiri kati ya Tanga na Lushoto
kugongana na lori la mizigo aina ya Scania iliyokuwa ikitokea jijini Dar
es salaam.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoa wa Tanga, Juma Ndaki ajali hiyo imetokea leo eneo la Mkanyageni
majira ya saa 1 asubuhi wakati magari hayo yakijaribu kupishana.
Alisema ajali hiyo ilihusisha coster
yenye namba T 410 BJD iliyokuwa ikiendeshwa na Bakari Musa na lori lenye
namba za usajili T 645 LBJ lenye tela namba T 605 ABJ lililokuwa
likendeshwa na Benjamin Abeid.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Tanga, Dk. Aisha Mahita akizungumzia ajali hiyo alisema maiti na
majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali Teule ya wilaya la
Muheza.
Hata hivyo Dk. Mahita alisema
majeruhi waliopokelewa katika Hospitalini hapo Teule ni 25 ambapo kati
yao 19 ni wanaume na 6 ni wanawake.
No comments:
Post a Comment