ANGALIA VIDEO MASHAMBULIZI YA ANGA YA WAMAREKENI DHIDI YA ISIS NCHINI SYRIA
Majeshi
ya Marekani yameanza rasmi mashambulizi ya anga nchini Syria yakilenga
kundi la kigaidi la ISIS (Islamic State of Iraq and Syria).Makao
Makuu ya Ulinzi ya Marekani yameeleza kuwa wanafanya mashambulizi ya
mchanganyiko kwa kutumia mabomu, wapiganaji wa ardhini pamoja na majeshi
ya Anga kutoka nchi za Mashariki ya Kati zinazowaunga mkono.Lakini
habari za mashambulizi yaliyoanza zilitolewa na raia wa Syria
aliyetweet kuhusu kile anachokisikia katika mji aliopo wa Raqqa ambako
kuna makao makuu ya kundi hilo.
Mtu huyo anaetumia
jina la Abdulkader Hariri aliandika kuwa milipuko mikubwa imelenga
makao makuu ya ISIS na kwamba anga lote limejaa ndege za kivita na
drones.
Baadae Agency ya wanaharakati nchini Syria ilipost video fupi inayoonesha kwa mbali mashambulizi.
No comments:
Post a Comment