Pages

September 21, 2014

AFANDE SELE AWAASA WASANII KUUNGANA NA KUWA KITU KIMOJA,AWATAKA KUACHA TABIA YA KUBAGUANA.

 Baadhi ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2014 lenye kauli mbiu (sambaza upendo) wakiwasili mapema leo mchana nyumbani kwa Mama Mkwe wa Afande Sele,mtaa wa Amani mjini Morogoro kwa madhumuni ya kutoa pole kwa Afande Sele pamoja na Familia ya marehemu ya aliyekuwa Mzazi mwenzake Afande Sele,Marehemu Asha aliyetambulika zaidi kwa jina la Mama Tunda,ambaye leo anatimiza siku Arobaini tangu afariki na kuzikwa.
 Baadhi ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza jioni ya leo katika tamasha la Fiesta pichani wakiwa katika suala zima la kufariji wakiwemo Wazee wa eneo hilo ambao walifika kwenye shughuli ya kutimiza siku Arobaini tangu kufariki kwa mke wa Afande Sele aliyekuwa akiishi nae kwa takribani miaka 17 na kufanikiwa kupata watoto wawili ambao ni Tunda na Asante sanaa.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Mo Music anaetamba na wimbo wake wa Basi nenda unaofanya vyema katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini,akitoa mkono wa pole kwa Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akitoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Weusi,Joe Makini akitoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana.
 Mtoto wa kwanza wa Afande Sele,aitwaye Tunda akisalimiana na baadhi ya wasanii waliofika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana,ambapo Marehemu Mama Tunda leo anatimiza siku arobaini tangu kufariki kwake.
 Afande Sele akiwa na watoto wake wawili alioachiwa na Marehemu Mama Tunda,ambao ni Tunda na Asante Sanaa wakiwa wamepozi mbele ya Camera ya Globu ya jamii mapema leo mchana.
  Afande Sele akiwa na watoto wake wawili alioachiwa na Marehemu Mama Tunda,ambao ni Tunda na Asante Sanaa wakiwa wamepozi mbele ya Camera ya Globu ya jamii mapema leo mchana.
 Baadhi ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2014,ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakiwa na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa Familia ya marehemu Mama tunda,ambapo leo inafanyika arobaini yake,mtaa wa Amani mjini Morogoro.
 Baadhi ya wasanii wakiwa wametulia wakitafakari yao. 
 Pichani kulinia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Leo Tena kutoka Clouds FM,Da Husna akiwa na mtoto wa Afande Sele,aitwaye Tunda.
 Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Mkali wa Rhymes Afande Sele akiushukuru Uongozi wa Clouds Media Group sambamba na kuwashukuru Wasanii hao waliofika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana,ambapo Marehemu Mama Tunda leo anatimiza siku arobaini tangu kufariki kwake.
 Afande Sele akizungumza kwa kuwataka wasanii kuungana na kuwa kitu kimoja katika shida na raha,kuacha tabia ya kubaguana na kujengeana chuki ambako kumekuwa ni sehemu ya kuufanya muziki wao na mambo yao mengi yasifanikiwe ipasavyo,Hivyo amewashauri wasanii kuwa na roho ya kupendana na kufanya kazi zao kwa kujituma na ubunifu ili tasnia ya muziki iweze kufika mbali zaidi.
 Ommy Dimpoz katika picha ya pamoja 
 Da Husna wa Leo Tena ya Clouds FM katika picha ya pamoja
Afande Sele akishoo love na Ommy Dimpoz.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...