Sista Anna Enzi za uhai wake.
Msiba
wa sista Anna Peterson umeibua simanzi si kwa familia yake tu bali kwa
wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe alipokuwa akifanya kazi za
kijamii tangu
ujana wake.
Hayo
yamebainika wakati wa ibaada maalum ya kumkumbuka iliyofanyika hii leo
katika kanisa la KKKT usharika wa Amani Bulongwa, ibaada iliyoongozwa na
baba askofu wa dayosisi ya kusini kati Levis Sanga, Askofu Mstaafu Dkt.
Solomon Swallo na Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa pamoja na msaidizi
wa askofu Philemon kahuka.
Akihubiri
katika ibaada hiyo maalum Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa amesema
marehemu alikuwa akifanya kazi zake kwa mkono wa dayosisi ya kusini kati
tangu enzi za ujana wake bila ubaguzi ingawa yeye alikuwa mzaliwa wa
nchi ya Sweeden.
Askofu mstaafu Manyiewa akihubiri ibadani hapo.
Amesema
amemfahamu toka 1969 na hadi anafikwa na umauti alikuwa akisaidia
watoto yatima, wajane, wagane na walemavu wote na hata wasiojiweza na
kusisitiza kuwa kanisa haliwezi kumsahau kamwe.
Akielezea
historia ya marehemu Askofu mstaafu Dkt Solomon Swallo amesema Sista
Anna alikuwa akifanya kazi zake kwa kujituma bila kujali ugumu wa kazi
uliokuwepo kwa kipindi hicho hasa ubovu wa barabara na ugumu wa
kuwafikia wananchi kutokana na tabu ya usafiri.
Askofu mstaafu Dkt Solomon Swallo.
Dkt
Swallo amesema alikuwa akisisitiza kuwa Mungu ndiye aliyemtuma kufanya
kazi Bulongwa Makete na si Binadamu hivyo haoni shida kutumikia jamii ya
Makete toka ujana hadi uzee wake.
Dkt Nicodemas Kikoti.
Kwa
upande wake Kaimu Mganga mkuu hospitali ya Bulongwa Dkt Nicodemas Kikoti
amesema marehemu pia alikuwa akifanya kazi na hospitali hiyo pamoja na
jamii ikiwemo kusomesha watoto yatima kutoka shule ya awali mpaka vyuo,
kuwajengea nyumba wasiojiweza, kuhudumia wajane, kusaidia vifaa vya
umeme pamoja na kujenga makao ya kituo cha watoto yatima Bulongwa.
Mch. Dkt Phares Ilomo.
Naye
Mch. Dkt Phares Ilomo kutoka chuo Kikuu cha Iringa amesema yupo tayari
kuandika kitabu cha kuelezea historia ya marehemu Sista Anna kwa
kushirikiana na viongozi wengine wa kanisa na washarika kuchangia
gharama ili kitabu hicho kichapishwe na kuzalishwa kwa faida ya vizazi
vijavyo ikiwemo kukiweka katika maktaba ya chuo chake.
Waziri
wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mahenge ambaye
pia ni mbunge wa jimbo la Makete akitoa salamu za rambirambi amesema
marehemu alikuwa akifanya shughuli ambazo kimsingi zilitakiwa kufanywa
na serikali hivyo wema wake kwa jamii ya Makete hauna mfano.
Waziri
wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dkt Binilith Mahenge ambaye
pia ni mbunge wa jimbo la Makete akitoa salamu za rambirambi.
Amesema
njia pekee ya kumuenzi ni kufanya yale aliyoyapenda huku akisisitiza
kuwa serikali itashirikiana na kanisa kuendeleza kazi zote alizoziacha
Sista Anna.
Askofu wa dayosisi ya kusiki kati Levis Sanga.
Askofu
wa dayosisi ya kusiki kati Levis Sanga ametangaza tarehe 26 Juni kila
mwaka kuwa ni siku maalum kikanisa ya kumkumbuka marehemu sista Anna
hivyo jamii inashauriwa kufika kwenye kituo cha watoto yatima Bulongwa
kwa ajili ya kuwatembelea na siku hiyo itakuwa ikifanyika ibaada maalum
kwa ajili ya marehemu.
Sista
Anna Peterson amefariki Juni 26 mwaka huu nchini Sweeden alipokwenda kwa
ajili ya matibabu na amezikwa leo hii nchini humo, na hapa Makete
alikokuwa akiishi toka ujana wake imefanyika ibaada maalumu ya
kumkumbuka.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Sista Anna Peterson, Amen.
Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete
No comments:
Post a Comment