NIkama jina la wimbo wake mpya wa Mdogo Mdogo ambao ndani yake kuna kikorombwezo ‘mwendawazimu kaingiaje’, ndiyo hali iliyotokea kwenye futari ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alipofuturisha nyumbani kwake ambapo pombe zilitibua shughuli nzima.
Pamoja
na kufuturisha, pia Diamond alimwandalia pati mama yake mzazi, Sanura
Kassim a.k.a Sandra aliyekuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa.
WAALIKWA WATAZAMANA
Katika tukio hilo lililojiri nyumbani kwa
staa huyo maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar mapema wiki hii, wageni
waalikwa walijikuta wakitazamana na kuhoji uhalali wa chupa za pombe
kuwepo ndani katika sehemu ambayo walitakiwa kufanyia dua.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya
wanahabari wetu, baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo maustadhi
walioshangazwa na jambo hilo, walihoji kuwa kulikuwa na ulazima gani au
kilishindikana nini wahusika kuziondoa pombe hizo halafu wazirudishe
baadaye.
Pombe zilizonaswa.
“Unajua huu ni mwezi wa imani zaidi, sasa
linapotokea suala la ibada kama hili la kufuturisha basi kuna vitu
vingine unatakiwa uvifiche ikiwezekana uachane navyo kabisa.
“Sioni sababu ya zile pombe kuachwa pale
sebuleni kila aliyeingia ndani kula keki anakutana nazo uso kwa uso,”
alisikika akilalama mmoja wa waumini wa Dini ya Kiislamu walioalikwa.
POMBE ZAONDOLEWA
Hata hivyo, pombe hizo kali ziliondolewa mahali hapo mara moja kisha shughuli ikaendelea.
SHAMPEINI YA WEMA YATILIWA SHAKA
Katika kuendelea kuweka walakini, muumini
mwingine alikwenda mbali zaidi na kuitilia shaka shampeini
iliyofunguliwa kuwa ni nani aliichunguza kama ilikuwa na kilevi au la!.
Maustadhi wakielekea kwenye futari.
“Wakati shampeini inaletwa niliona,
aliileta kijana mmoja namjua kwa jina la James ambaye ndiye aliyempatia
Babu Tale (meneja wa Diamond), naye akampatia Wema Sepetu (laazizi wa
Diamond).
“Sidhani kama walikuwa na muda wa kusoma
kama ina kilevi au la ndiyo maana baada ya Wema kuifungua watu
waliikataa wakidhani ina kilevi hivyo ikamdodea mrembo huyo kwani
ilidaiwa kama ilikuwa na kilevi ni jambo baya kwa mwezi mtukufu.
WAINYWA WATATU
“Walioinywa ni watatu tu, Wema, mama
Diamond na dada yake Diamond, Esma Platnumz,” alisema mmoja wa waumini
hao akitoa hoja juu ya kuitilia shaka shampeini hiyo ambayo waandishi
wetu hawakupata nafasi ya kusoma maelezo yake.
Wageni waalikwa wakipata futari.
MSIKIE BABU TALE
Baada ya kupata maelezo hayo, Ijumaa
lilijaribu kuhoji kwa wahusika ambapo Meneja wa Diamond, Babu Tale
alisema kuwa licha ya kutokaguliwa kwa Shampeini lakini haikuwa na
kilevi.
“Shampeini haikuwa na kilevi, lakini kuhusu suala la chupa za pombe pale sebuleni, ule ulikuwa ni urembo tu ambao upo siku zote.
“Hata
mama Diamond akitaka kuswali huwa anasogeza meza na kufanya ibada yake
ya swala, zile chupa zinakuwa zipo palepale ila kwa Wabongo siku zote
wapo kwa ajili ya kuwakatisha watu tamaa tu.“Zile chupa huwa zipo kila
siku zimekaa tu kama nilivyosema kuwa ni urembo,” alisema Babu Tale.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
DIAMOND HAKUWEPO
Katika shughuli hiyo, pamoja na kwamba
alikuwa nchini Marekani, Diamond alimzawadia mama yake gari aina ya
Toyota Lexus Harrier lililogharimu Sh. milioni 38.1 alilokabidhiwa na
Babu Tale.
No comments:
Post a Comment