Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Fredrick Msigala akizungumza na wanahabari
mara baada ya Mkutano wao na Mtandao wa Wanawake na Katiba uliofanyika
katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa
majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika
majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akiongoza majadiliano
katika Mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mtandao wa
Wanawake na Katiba. Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa
majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika
majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa
majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika
majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa
majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika
majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam.
WAJUMBE wa
Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano
uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wameahidi kupaza sauti
kupigania masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia pamoja na
kusimamia usawa kwa jamii yote juu ya mgawanyo wa rasilimali ardhi,
elimu, uongozi na huduma za kijamii.
Kauli
hiyo imetolewa leo na baadhi ya wajumbe hao walipokuwa wakizungumza na
waandishi wa habari, katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es
Salaam eneo unapofanyika mkutano huo uliomalizika leo jioni.
Mjumbe
wa Bunge Maalum, Valerie Msoka alisema majadiliano walioshiriki
yamewawezesha wajumbe kurudi katika majadiliano ya awamu ya pili wakiwa
na nguvu mpya huku wakiyapa kipaumbele na kuhakikisha kuna usawa katika
masuala ya ardhi, elimu, rasilimali, uongozi na huduma za kijamii.
Alisema
kwa muda wa mwanzo ambao wajumbe walipata kuhudhuria na kujadili baadhi
ya ibara wamepata uzoefu kidogo jambo ambalo kwa kipindi cha pili
litawasaidia kuongeza ujasiri wa kuendeleza hoja zao za msingi zikiwemo
walizoshiriki kuzijadili katika mkutano huo.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Bunge Maalum, Fedrick Msigala alisema mkutano huo
umewawezesha wajumbe kujenga zaidi uelewa juu ya masuala ya usawa wa
jinsia na kuangalia namna wajumbe wanaweza kuyatetea kuingizwa kwenye
mchakato wa uundaji katiba mpya unaoendelea.
“…Mimi
kama mwakilishi wa walemavu natambua namna ambayo wanawake walemavu
wanavyo athirika na vitendo vya ukatili na manyanyaso yote ambayo
wanakumbana nayo…sasa semina kama hii inatupa taarifa na uwezo pia wa
kujenga hoja katika kutetea usawa wa kijinsia kuingizwa vizuri kwenye
ibara mbalimbali husika kwenye Katiba Mpya,” alisema Msigala.
Naye
mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya alisema majadiliano
hayo kati ya Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba na Wajumbe wa Mtandao wa
Wanawake na Katiba ni nafasi muhimu kwani inawakumbusha wajumbe kupaza
sauti juu ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia kuingizwa kwenye
sheria mama ya nchi ambayo ni katiba.
Alisema
masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia yakiingizwa katika
jamii yataziwezesha mamlaka husika kuwajibika na taasisi husika
kusimamia kwa uhakika na kuziwajibisha pale masuala hayo yanaposhindwa
kutekelezwa kwa mujibu wa maelekezo.
“…Muhimu
pia ni kutambua umuhimu wa kusimika suala la usawa wa kijinsia kwenye
katiba ni kutokana na ukweli kwamba wanawake wanahusika katika
kulikamilisha taifa la Tanzania na wanamchango mkubwa licha ya mfumo
kuendelea kuwabana katika fursa mbalimbali,” alisema Bi. Mallya.
Alisema
sasa umefika wakati fikra potofu zitokomezwe ambazo zimekuwa
zikiendelea kuwabana wanawake kwamba hawawezi na kuambulia nafasi
ndogondogo maeneo anuai ya vyombo vya maamuzi ngazi zote.
“Nafasi
kama hii ya kuwezesha Wajumbe wa Bunge la Katiba waweze kuendelea
kuyabeba haya masuala katika mjadala utakaoendelea ni muhimu…na kwetu
sisi tunachotegemea ni kwamba haya masuala yataendelea kuwa ni sehemu ya
msingi katika majadiliano yanayoendelea kule bungeni, tunawaomba
waandishi wa habari waendelee kuzipa nafasi hizi hoja na tunawapongeza
pia kwa kutuunga mkono,” alisema Bi. Mallya.
Mkutano
huo umetoka na maadhimio ambayo wajumbe wataendelea kuyafanyia kazi,
ikiwemo washiriki kuendelea kuwasiliana na kupanua wingo wa kupaza sauti
juu ya hoja walizozijadili na kuyashirikisha makundi mengine katika
kupaza sauti ili hoja zilizojadiliwa zipate nafasi ya kuingizwa kwenye
mchakato.
No comments:
Post a Comment