Pages

July 26, 2014

MAANDALIZI YA MAONESHO YA KILIMO NA MIFUGO KANDA YA KASKAZINI(TASO),ARUSHA YAPAMBA MOTO

Msimamizi wa Kituo kituo cha kueneza teknolojia ya kilimo Kanda ya Kaskazini, Ernest Elias akifafanua jambo kwenye bustani ya mbogamboga.



Mdau wa Sekta ya Kilimo cha Nyanya akiangalia ubora wake kwenye bustani ya Kampuni ya Monsanto

Msimamizi wa Kituo kituo cha kueneza Teknolojia ya kilimo, Kanda ya Kaskazini, Ernest Elias akionesha bustani ya viazi.

Mtaalamu wa Kilimo kwenye bustani ya Halmashauri ya jiji la Arusha,Ester akionesha zao la Mtama

Mtaalamu wa Kilimo kwenye bustani ya Halmashauri ya wilaya ya Monduli akielezea umuhimu wa zao la Ngano






Arusha.
Msimamizi wa Kituo kituo cha kueneza teknolojia ya kilimo kanda ya kaskazini, Ernest Elias amesema kuwa teknolojia mpya ya kilimo cha mbogamboga itawasaidia wakulima kuimarisha lishe na kuongeza kipato.


Akizungumzia teknolojia hiyo ya mbegu za mboga mboga za mnafu na mchicha zilizozalishwa na kituo cha Utafiti cha Hoticulture Tengeru zinazoweza kukua kwa wingi katika eneo dogo na pia zina majani mapana.


Ernest amesema kuwa mbegu hizo ziligunduliwa mwaka 2010 na kuanza kutumiwa na wakulima na pia ni teknolojia asilia.


Mbegu hizo za asili ambazo zimeboreshwa zilizogunduliwa na watafiti wa ndani ya nchi za mnafu zimepewa majina ya Nduruma  na Olevolosi huku mbegu za mchicha zikiitwa madira 1 na madira 2.


"Unaweza kuziotesha katika eneo dogo na kuvuna mboga nyingi zinafaa katika maeneo yenye ardhi ndogo hata kwa waliopangisha mfano sisi kwenye vipando vyetu ambavyo tunaviandaa kwa ajili ya maonyesho ya nane nane tumeotesha mita za mraba 8 ni mboga nyingi" alisema Ernest


Amewataka wakulima watumie teknolojia ili kufanya kilimo chenye tija kinachoweza kuinua uchumi wao na kuondokana na umasikini.


Mbali na Kilimo cha mboga mboga wanajihusisha maonyesho ya  kilimo cha mahindi,mtama,ngano na viazi vitamu ambapo kwa mwaka jana wamesambaza vipando 95000 katika mikoa mbali mbali.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...