Pages

July 11, 2014

CHINA YASHUTUMIWA KUTOA SILAHA ZA KIVITA KWA SUDAN KUSINI ZA DOLA 38 MILIONI.


Sudan Kusini bado inakabiliwa na hali tete licha ya mkataba wa amani kutiwa saini.

Inaripotiwa kuwa China imetuma silaha zenye thamani ya dola milioni 38 nchini Sudan Kusini licha ya nchi hiyo kukabiliwa na mzozo ambao huenda utaitumbukiza katika baa la njaa.

Nyaraka zilizogunduliwa na wataalamu wa masuala ya ulinzi zinaonyesha kuwa makombora, bunduki za rashasha na risasi viliwasili nchini Sudan Kusini mwezi uliopita kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Wanadiplomasia wanakadiria kuwa Sudan Kusini inatumia mamilioni ya dola kwa ulinzi.

Kwingineko, muungano wa ulaya umewawekea vikwazo viongozi na kupiga tanji mali ya wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo kwa tuhuma za kukiuka makubaliano ya kusitisha vita ambayo yangeleta mazingira ya amani na kuziia mauaji ya maelfu ya wanachi.

Baraza la Muungano huo, halikuwataja wawili hao katika taarifa yao wala kutaja pande wanazounga mkono. 

Marekani imechukua hatua sawa na hizo dhidi ya viongozi kutoka pande zinazozozana. 

Vita vilizuka mjini Juba Disemba mwaka jana kati ya serikali na wapiganaji wa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.

Mgogoro huo bila shaka umetonesha kidonda katika taifa hilo changa zaidi duniani tangu kujitawala mwaka 2011.BCC.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...