Msemaji wa serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa
kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa
kujipiga risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha
ofisi za ubalozi huo.
Mwambene alisema kuwa mpaka sasa haijafahamika kifo cha balozi huyo
kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu katika ubalozi huo
wamesema kuwa walisikia mlio wa risasi chumbani kwake, na walipojaribu
kufungua mlango ulikuwa umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja mlango
huo na kufanikiwa kumkuta balozi yupo katika hali ya mbaya.
Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.
Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote wa
kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya
mazishi.
No comments:
Post a Comment