Mwili
wa Mawazo Wilbard Kazungu (31) ukiwa nyumbani kwake ukining'inia
baada ya kujinyonga katika chumba cha kulala watoto wake .
|
Eneo la chumba ambako alikaa kitandani na kunywa dawa ya kuoshea mifugo kisha kupanda stuli na kujitundika kamba
|
Vijana
walio kuwa na ukaribu na marehemu wakiwemo ndugu zake wakiubeba mwili
wa marehemu kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi chini ya jeshi la polisi
|
Wananchi wakiwa mbele ya nyumba ya marehemu Mawazo katika kushuhudia mwili ukiondolewa kwenye kamba kwenye chumba alikojinyongea
|
Wananchi wakiwa katika tukio la Mwazo Kazungu aliyejinyonga wakitafakari matukio ya kujinyonga wilayani Ngara
|
Wananchi
wakiwa katika nje ya nyumba ya Marehemu Mawazo Kazungu wakizungumzia
maisha yake wakati wa uhai wake kabla hajajinyonga.
Mwandishi Wetu,NGARA |
Kijana
mmoja mkazi wa kijiji cha Mukaliza wilayani Ngara mkoani Kagera
aliyetambulika kwa jina la Mawazo Wilbard Kazungu (31) juzi Juni 2014
amekutwa amejinyonga nyumbani kwake katika chumba cha kulala watoto wake.
Afisa
mtendaji wa kijiji cha Mukaliza, Joseph Festo amesema kijana huyo
alijinyonga kwa kutumia kamba ya kufungia mifugo aina ya Katani na kabla
ya kujitia kitanzi alianza kunywa dawa ya kuoshea ng'ombe na ndipo
aliingiza shingo katika fundo la kamba ikitokea katika paa la nyumba
yake.
Festo
alisema tukio hilo lilitokea saa 6 mchana ambapo mke wake alikuwa
amekwenda shambani na aliporejea alimkuta mumewe akining'inia chumbani
akiwa tayari ameshafariki huku chini ya kitanda cha watoto wao kukiwa na
kopo la dawa ya ng'ombe ambalo alilifungua na kunywa dawa hiyo.
Alidai kuwa katika maisha ya kijana huyo alikuwa ni mjasiliamali wa kuuza mifugo na mazao mbalimbali katika Kata ya Mabawe kwa kujiongezea kipato kiuchumi na alikuwa hajashtakiwa kwa dhuluma bali aliishi vema na wananchi wake pamoja na jamaa wakiwemo marafiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Mukaliza, Manase Rutegama amesema kuwa marehemu Mawazo wakati wa uhai wake hakuwahi kuwa na ugomvi wa kifamilia na alikuwa akifanya shughuli bila kuwa na migogoro yoyote.
"Viongozi na wanafamilia tumepokea kifo hicho kwa mshituko na katika kata ya mabawe wananchi walikuwa hawajapata kupata mtu aliyejinyonga na huyo kijana kaacha watoto watatu na mke mmoja".Alisema Rutegama.
Katika kutungua mwili wa marehemu kwenye kamba chini ya jeshi la polisi mganga mfawidhi wa kituo cha afya mabawe Juvent John alisema kamba ndiyo ilikatisha maisha yake baada ya kuziba mishipa ya damu na kukata mawasiliano ya kupumua.
Hata hivyo jeshi la polisi licha ya kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho limewataka wananchi kuwa na ulinzi shirikishi kuhakikisha kila mmoja anatambua shda za mwenzake na kutoa taarifa katikavyombo vya dola kwa yule aliye na maoni ya kutaka kujiondoa nafsi yake ama kufanya matukio ambayo ni makosa ya jinai.
Mmoja wa askari polisi jamii aliyetambulika kwa jina la Oscar alisema katika jeshi la plisi kuna dawati la ushauri nasaha kwani matukio ya kujinyonga wilayani Ngara yanazidi kuongezeka hasa kwa kuhusisha kundi la vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Alisema wanaobaki wakiteseka kutokana na matukio hayo ni akina mama na watoto na wazee waliokuwa wategemezi wa vijana hao na wananchi kwa imani zao hawana budi kusali pamoja kuomba Mungu kuepusha jinamizi hilo la watu kujinyonga.
No comments:
Post a Comment