Pages

June 30, 2014

UJUMBE WA CHAMA CHA WABUNGE WA JUMUIYA YA MADOLA WATEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE NA MANYARA LEO

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Thomas Kashililah(katikati)akiwa na Maafisa wa Bunge,Saidi Yakubu wakifurahia mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire leo ikiwa ni sehemu ya tathmini ya Mkutano wa Chama cha wabunge wa Jumuiya ya Madola(CPA)utakaofanyika jijini Arusha mwezi wa Julai,mwaka huu.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire,Stephano Qolli(wa pili kushoto)akitoa maelezo kwa Ujumbe wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya Madola(CPA)waliotembelea Hifadhi hiyo leo.

Mjumbe wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola tawi la Tanzania(CPA)Mh.Beatrice Shelukindo akizungumza jambo.

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa(Tanapa)akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola(CPA)tawi la Tanzania waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire leo.

Tembo ni wanyama maarufu katika Hifadhi ya Taifa Tarangire

Pundamilia nao huongeza uzuri wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...