Tabasamu kubwa: Giorgio Chiellini ameumia na adhabu aliyopewa Suarez kwa kumng`ata .
Imechapishwa Juni 27, 2014, saa 9:20 alasiri
BEKI wa Italia, Giorgio Chiellini amefunguka kutokana na adhabu aliyopewa Luis Suarez kwa kumng`ata.
Mshambuliaji
huyo wa Liverpool aling`ata kwa mara ya tatu katika maisha yake ya soka
baada ya kumshambulia Chiellini wa Italia na kumtia meno katika dakika
ya 80 ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi na kushuhudia Uruguay
ikishinda kwa bao 1-0.

Suarez amefungia miezi minne kutocheza soka baada ya kumtia meno Chiellini
Lakini kwa Italia kuwa nje ya mashindano, Chiellini anaamini adhabu ya Suarez ni kali sana , hivyo anampa pole.
"Moyoni
mwangu sina hisia za furaha, kisasi wala hasira dhidi ya Suarez
kutokana na tukio lile lililotokea uwanjani na yamekwisha". Aliposti
katika mtandao wake rasmi.
"Hasira
zangu kwasasa zimebaki kwenye mechi na matokeo. Ni wakati ambao
namuwazia Suarez pekee na familia yake kwasababu watakuwa kwenye wakati
mgumu sana".

Hapa
kitu cha meno tu: Suarez (kushoto) alinaswa na Kamera akimng`ata beki
wa Italia Giorgio Chiellini (kulia) kwenye mechi ya jumanne.
Maumivu: Chiellini akivua jezi yake kuonesha sehemu aliyong`atwa na Suarez wakati wa mechi yao ya kundi D mjini Natal.

إرسال تعليق