|
Kikundi cha ngoma kikitoa Burudani kabla ya pambano la Ngumi kuanza kati ya Bondia Alibaba Ramadhan wa Kilimanjaro na Roy Mbunda wa Ruvuma. |
|
Mgeni rasmi katika pambano hilo mkuu wa polisi wa wilaya OCD Deusdedit Kasindo akizungumza kabla ya kuanza kwa pambano la ngumi katika ya bondia Alibba na Roy Mbunda. |
|
Likafuata pambano la Bondia Massawe toka Kibosho . |
|
Akapambana na Bondia Rasta toka jijini Arusha. |
|
Bondia Masawe toka Kibosho akapewa Ushindi kwa kumtwanga KO Bondia Rasta. |
|
Bondia Rasta akifurahia ushindi. |
|
Ngumi zikapigwa kwa raund zote nne. |
|
Mabondia wote wakiwa hoi kama anavyoonekana Fredy George akivuliwa Groves. |
|
Bondia Pascaly Bruno akatangazwa mshindi . |
|
Baadae sasa likafuata pambano lililokuwa likisubiriwa na wengi ni la kuwania mkanda wa taifa kati ya Bondia Alibaba Ramadhan na Roy Mbunda. |
|
Pambano likaanza ndani ya round ya pili tu Bondia Alibaba anasukuma konde kwa bondia Roy Mbunda lililompeleka chini. |
|
Baadae Roy Mbunda akaamka akigugumia maumivu ya mguu akidai msuli wa paja umebana. |
|
Mwamuzi Chaku akalazimika kukatisha pambano kutokana na Bondia Mbunda kuda hatoweza endelea na pambano. |
|
Mashabiki nao walilipuka kwa kelele. |
|
Akanyooshwa viungo. |
|
Kisha akavalishwa mkanada wake wa Ubingwa akapata picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi pamoja na wadhamini. |
|
Akapongezwa Roy Mbunda. |
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment