MVUA ZALETA MADHARA MAKUBWA LUDEWA , MBUNGE FILIKUNJOMBE AKWAMA KUWAFIKIA WAPIGA KURA AKESHA AKIZIBUA BARABARA

Wananchi na  msafara  wa  mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe wakifungua barabara ya  Rupingu -Ludewa  iliyofunikwa na kifusi baada ya mvua kubwa  kunyesha kwa zaidi ya wiki moja mfululizo sasa barabara  hiyo  ipo katika matengenezo makubwa na TANROADS mkoa wa Njombe kwa kutegewa kiasi cha Tsh milioni 400
Gari la Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe  likipita kwa shida katika barabara ya Rupingu -Ludewa jana
Mbunge wa  Ludewa Deo Filikunjombe akkitazama sehemu ya barabara ya Rupingu – Ludewa  inayoporomoka kutokana na mvua  kubwa  zinazoendelea  kunyesha
Mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe akionyesha madhara ya  Mvua yaliyopelekea barabara ya Rupingu -Ludewa  kuharibika
Na Francis Godwin,Blog
MVUA kubwa  zinazoendelea  kunyesha  katika maeno  mbali  mbali ya  hapa  nchini  zimeendelea  kuleta  madhara  makubwa katika wilaya ya  Ludewa  mkoani Njombe baada  ya mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kukesha akifungua barabara   na  wananchi  wake baada ya kukwama  kuendelea  na ziara ya kuwatembelea   wapiga kura  wake wa  kata ya  Rupingu  kutokana na kifusi na miti  mkuporomoka na kuziba barabara  hiyo ya Ludewa – Rupingu .

Tukio   hilo  lilitokea  juzi  majira ya saa 3 asubuhi  wakati msafara wa  mbunge  huyo  wenye magari matatu  kujikuta  ukikwama katika  eneo la Mlima Rupingu kwenye  barabara ya Ludewa- Rupingu umbali wa Kilomita 15 hivi  kutoka mjini  Ludewa hali  iliyomlazimu mbunge  huyo na  viongozi mbali mbali wa CCM wilaya ya  Ludewa kuungana na  wananchi  waliokuwa  wakielekea kuzika  kufanya kazi ya  kuzibua  barabara  hiyo.

Wakizungumza na  mwandishi wa  habari hizi wananchi  wa Rupingu  ambao  walikuwa  wamekwama katika  eneo hilo kwa  zaidi ya  siku  tatu  na maiti  yao  iliyokuwa ikisafirishwa kwenda kijijini  walisema  kuwa  mvua hizo zimeendelea  kuleta madhara makubwa katika  barabara   hiyo na kuwa  wao  wamepata kukwama eneo hilo kwa  zaidi ya  siku tatu kutokana na maporomoko ya kifusi  katika barabara  hiyo.
Alisema John Haule  kuwa   uwezekano wa  wao kukamwa kwenda kuzika ulikuwa mkubwa  zaidi kama mbunge  wao asingekuwa katika  ziara  kuelekea Rupingu kwani kufanya  ziara kipindi hiki cha masika  kummemfanya mbunge  kujua  kero   hiyo.

“Kwanza  tunampongeza  sana mbunge  wetu Filikunjombe wabunge  waliopita  kipindi kama hiki cha mvua walikuwa  hawafiki  vijijini  zaidi ya  kuishia Ludewa mjini  ila yeye anafanya  ziara  wakati  wote na kuona changamoto mbali mbali ambazo  wananchi  wake  tumekuwa  tukizipata …. hivi ni kiongozi gani anakubali  kushuka katika gari lake na kuingia katika tope  kuchimba  kifusi pamoja na  wananchi wake….kweli Ludewa tumempata mbunge wa wananchi  kweli sio mbunge wa  kujitumikia yeye na familia  yake”
 Hata  hivyo alisema  barabara  hiyo ambayo  ipo chini ya  wakara wa barabara mkoa wa Njombe  imeendelea kuboreshwa  toka alipoingia Filikunjombe madarakani na mkoa wa Iringa  kugawanywa .
Kwa  upande  wake  mbunge Filikunjombe mbali  ya  kuwapa  pore  wafiwa hao na  wananchi wa Rupingu kwa kukosa barabara  kutokana na mvua  hizo bado  alipongeza  jitihada kubwa  zinazofanywa na uongozi wa TANROADS mkoa wa Njombe katika  kuzihudumia barabara  hizo kwani  alisema ubovu wa barabara   hiyo  unatokana na mvua kubwa zinazoendelea  kunyesha kama ambavyo maeneo mengine yanavyopata madhara  kama  hayo  .
Hivyo  alisema kwa upande wake anapongeza jitihada za TANROADS mkoa wa Njombe kwa  kuendelea  kuboresha barabara  hiyo  ya Rupingu-Ludewa ambapo kwa mwaka jana imeboresha kwa mamilioni ya shilingi na mwaka  huu imetengewa  zaidi ya Tsh milioni 400

Post a Comment

Previous Post Next Post