| Gari la Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe likipita kwa shida katika barabara ya Rupingu -Ludewa jana |
| Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akkitazama sehemu ya barabara ya Rupingu – Ludewa inayoporomoka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha |
| Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akionyesha madhara ya Mvua yaliyopelekea barabara ya Rupingu -Ludewa kuharibika |
Na Francis Godwin,Blog
MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeno mbali mbali ya hapa nchini zimeendelea kuleta madhara makubwa katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kukesha akifungua barabara na wananchi wake baada ya kukwama kuendelea na ziara ya kuwatembelea wapiga kura wake wa kata ya Rupingu kutokana na kifusi na miti mkuporomoka na kuziba barabara hiyo ya Ludewa – Rupingu .
Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3 asubuhi wakati msafara wa mbunge huyo wenye magari matatu kujikuta ukikwama katika eneo la Mlima Rupingu kwenye barabara ya Ludewa- Rupingu umbali wa Kilomita 15 hivi kutoka mjini Ludewa hali iliyomlazimu mbunge huyo na viongozi mbali mbali wa CCM wilaya ya Ludewa kuungana na wananchi waliokuwa wakielekea kuzika kufanya kazi ya kuzibua barabara hiyo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wananchi wa Rupingu ambao walikuwa wamekwama katika eneo hilo kwa zaidi ya siku tatu na maiti yao iliyokuwa ikisafirishwa kwenda kijijini walisema kuwa mvua hizo zimeendelea kuleta madhara makubwa katika barabara hiyo na kuwa wao wamepata kukwama eneo hilo kwa zaidi ya siku tatu kutokana na maporomoko ya kifusi katika barabara hiyo.
Alisema John Haule kuwa uwezekano wa wao kukamwa kwenda kuzika ulikuwa mkubwa zaidi kama mbunge wao asingekuwa katika ziara kuelekea Rupingu kwani kufanya ziara kipindi hiki cha masika kummemfanya mbunge kujua kero hiyo.
“Kwanza tunampongeza sana mbunge wetu Filikunjombe wabunge waliopita kipindi kama hiki cha mvua walikuwa hawafiki vijijini zaidi ya kuishia Ludewa mjini ila yeye anafanya ziara wakati wote na kuona changamoto mbali mbali ambazo wananchi wake tumekuwa tukizipata …. hivi ni kiongozi gani anakubali kushuka katika gari lake na kuingia katika tope kuchimba kifusi pamoja na wananchi wake….kweli Ludewa tumempata mbunge wa wananchi kweli sio mbunge wa kujitumikia yeye na familia yake”
Hata hivyo alisema barabara hiyo ambayo ipo chini ya wakara wa barabara mkoa wa Njombe imeendelea kuboreshwa toka alipoingia Filikunjombe madarakani na mkoa wa Iringa kugawanywa .
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe mbali ya kuwapa pore wafiwa hao na wananchi wa Rupingu kwa kukosa barabara kutokana na mvua hizo bado alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na uongozi wa TANROADS mkoa wa Njombe katika kuzihudumia barabara hizo kwani alisema ubovu wa barabara hiyo unatokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kama ambavyo maeneo mengine yanavyopata madhara kama hayo .
Hivyo alisema kwa upande wake anapongeza jitihada za TANROADS mkoa wa Njombe kwa kuendelea kuboresha barabara hiyo ya Rupingu-Ludewa ambapo kwa mwaka jana imeboresha kwa mamilioni ya shilingi na mwaka huu imetengewa zaidi ya Tsh milioni 400

إرسال تعليق