![]() |
| Mkazi wa Kijiji cha Chemchem akilalama kwenye mkutano wa kumpinga mwekezaji |
![]() |
| Wananchi wenye hasira kali wakichoma uzio wa muda. |
Filbert
Rweyemamu,Karatu
Wananchi wenye hasira katika Kijiji cha
Chemchem,Kata ya Rhotia wilayani Karatu wamevamia eneo la mwekezaji mzawa
,Samwel Kastuli na kuharibu uzio wa muda na banda lililokua linalohifadhi vifaa
vya ujenzi kwa kudai eneo hilo la zaidi ya heka 14 sio lake bali ni mali ya
Kijiji kwaajili ya malisho ya mifugo.
Katika mkutano uliofanyika juzi kwenye
eneo linalobishaniwa na pande hizo zaidi ya wananchi 300 walikuwepo na kumwomba
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,Profesa Anna Tibaijuka kuingilia kati mgogoro huo ili kuepusha madhara
yanayoweza kutokea.
Mmoja wa wananchi hao,Hiiti Tlatlaa
alisema hawatakubali eneo hilo lililopakana na Hifadhi ya taifa ya Ziwa Manyara
lichukuliwe na mwekezaji yeyote wakati lilitengwa kwa shughuli za mifugo ya
wanakijiji wote na bado kuna mahitaji ya ardhi kwaajili ya vijana
wao.
Mwenyekiti wa kwanza wa Kijiji hicho
kiliposajiliwa mwaka 1975,Mohe Bura na Martina Kastuli walidai mwekezaji
amezungushia uzio kwenye eneo la zaidi ya heka 100 wakati mwekezaji anadai ni
eneo la heka 14,wanatambua wawekezaji wawili waliopewa ardhi kwa halali ambao ni
Bulk Oil heka 80 na Zapata heka 7 na si vinginevyo.
“Kijiji chetu hakina uongozi wa tangu
mwaka 2011 kwasababu ya viongozi walafi tuliowatimua madarakani ambao ni
Mwenyekiti Tlatlaa Bura na Mtendaji wake wanaojitafutia maslahi yao bila
kuwashilikisha wananchi tunaomba viongozi wetu wa ngazi ya juu watusaidie
kuondoa kero hii,”alisema Bura
Kwa upande wake mwekezaji huyo,Samwel
Kastuli alidai ameshachukua hatua za kisheria dhidi ya wananchi waliofanya
uharibifu wa mali zake zikiwemo uporaji wa Saruji,Nondo na vifaa vingine
kwaajili ya ujenzi wa hoteli ya kitalii.
Alisema ana hati halali za ununuzi wa
eneo hilo kutoka kwa mkazi wa Kijiji hicho,Shauli Hhansa na amesikitishwa na
uamuzi wa baadhi ya wananchi hao kwani mradi huo utakapokamilika utatoa ajira
kwao.



إرسال تعليق