Mwanachama wa Mfuko wa LAPF kutoka mkoani Mtwara ambaye ni mstaafu,Bi Aisha Sufian akitoa ushuhuda wake jinsi alivyonufaika na mfuko huo.Picha zote na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
MFUKO wa Pesheni wa LAPF umepewa muda wa kuangalia njia mbadala ya kutoa mikopo ya nyumba kwa wanancha wake,kabla ya kustaafu ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuepukana na wimbi la umaskini.
Aliyasema hayo jijini Arusha ,Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Tawala za mikoa na serikali za mitaa,Hawa Ghasia wakati akifungua mfuko wa 6 wa mwakawa Mfuko wa Pesheni wa LAPF.
Alisema mfuko huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kujali wanacham wake lakini amewataka wajumbe wa LAPF kujadili changamoto zinazowakabili kwa kina ili wanachama wanapopewa pensheni wazitumie vizuri.
Hata hivyo pamoja na hayo amewaagiza waajiri nchini kuwapatia elimu waajiri wapya ili waweze kuchagua mifuko wanayohitaji kujiunga,ili kuepukana na changamoto iliyopo katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
“nawaagiza waajiri nchini angalieni namna ya kuwapatia elimu wafanya kazi wapya katika mahali mlipo,na muangalie namna ya kuwapatia mikopo wajumbe wa LAPF katika mabenki ili kujiajiri kabla ya kastaafu kwamaana huko ndiko watakapo pata uzoefu wakutosha kabla ya ile miak 55 mnayoihitaji ninyi” alisema Ghasia.
Alisema LAPF wanatakiwa kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa fao la elimu haraka iwezekanavyo,kwani ameshataarifiwa kuwa fao hili limeanza kushughulikiwa kuanzia mwaka jana.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo ambao ni wa siku mbili Mwenyekiti wa bodi ya LAPF Profesa Hassa Mlawa,alisema LAPF tangu mwaka 2009/10 ukifanya vizuri kwa kupata hati safi zaidi ya miaka mitano na katika kipindi cha miaka mine mfuko umepewa tuzo ya na bodi ya wakaguzi na wahasibu (NBAA).
Naye mkurugenzi mkuu wa LAPF Elihudi Sanga alisema mfuko huo katika mwaka wa fedha 2012/2013 mfuko huo uliandikisha wanachama takribani 17,840 ikilinganishwa na wanachama 12,466 walioandikishwa mwaka 2011/2012 ambapo katika mwaka wa fedha 2013/2014 wanatarajia kuandikisha wanachama wapya 20,000 toka sekta zote za kiuchumi.
Mkutano huo utajadili changamoto mbali,kubadilishana mawazo na njia mbalimbali za kuboresha ,huku kauli mbiu ya mwaka huu ikisema, kukidhi kwa mafao ya wastaafu ,changamoto na njia za kuboresha.
|
Post a Comment