MFUKO WA LAPF WAZIDI KUWANUFAISHA WANACHAMA WAKE,WANACHAMA WAONGEZEKA HADI 17,000

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Hawa Ghasia(kushoto)akisalimiana na maafisa wa Mfuko wa LAPF  leo jijini Arusha kabla ya kufungua mkutano wa sita wa wadau wa mfuko huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Hawa Ghasia(kushoto)akisalimiana na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Mfuko wa LAPF,Amina Khasim  leo jijini Arusha kabla ya kufungua mkutano wa sita wa Wadau wa Mfuko huo.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Hawa Ghasia(katikati)akiwa na Waziri wa Kazi na Ajira(kulia kwake)Gaudensia Kabaka akiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC kufungua mkutano wa Sita wa Wadau wa Mfuko wa LAPF leo jijini Arusha,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa LAPF,Eliudi Sanga.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Hawa Ghasia akifungua mkutano wa Sita wa Wadau wa Mfuko wa LAPF leo jijini Arusha.


Wajumbe wa mkutano wa Sita wa Wadau wa LAPF wakifatilia kwa makini.

Wajumbe wa mkutano wa Sita wa Wadau wa LAPF wakifatilia kwa makini.

Mmoja wa wajumbe akisoma gazeti la Mwananchi kabla mkutano kuanza.

Mmoja wa wajumbe akisoma gazeti la Mwananchi kabla mkutano kuanza.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Hawa Ghasia(kulia)akimkabidhi zawadi ya uchangiaji mzuri Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Muleba mkoani Kagera,Oswald Rwezahula katika mkutano wa Sita wa Wadau wa Mfuko wa LAPF leo jijini Arusha.

Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka(kushoto)akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa LAPF,Profesa Asa Mlawa.

Wabunge waliohudhuria mkutano wa LAPF wakiteta jambo

Mwanachama wa Mfuko wa LAPF kutoka mkoani Mtwara ambaye ni mstaafu,Bi Aisha Sufian akitoa ushuhuda wake jinsi alivyonufaika na mfuko huo.Picha zote na www.rweyemamuinfo.blogspot.com


MFUKO wa Pesheni  wa LAPF umepewa muda wa kuangalia njia mbadala ya kutoa mikopo ya nyumba kwa wanancha wake,kabla ya kustaafu ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuepukana na wimbi la umaskini.
 
Aliyasema hayo  jijini Arusha ,Waziri  wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Tawala za mikoa na serikali za mitaa,Hawa Ghasia wakati akifungua mfuko wa 6 wa mwakawa Mfuko wa Pesheni  wa LAPF.
Alisema mfuko huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kujali
wanacham wake lakini amewataka wajumbe wa  LAPF kujadili changamoto
zinazowakabili kwa kina ili wanachama wanapopewa pensheni wazitumie
vizuri.
Hata hivyo pamoja na hayo amewaagiza waajiri nchini kuwapatia elimu
waajiri wapya ili waweze kuchagua mifuko wanayohitaji kujiunga,ili
kuepukana na changamoto iliyopo katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
“nawaagiza waajiri nchini angalieni namna ya kuwapatia elimu wafanya
kazi wapya katika mahali mlipo,na muangalie namna ya kuwapatia mikopo
wajumbe wa LAPF  katika mabenki ili kujiajiri kabla ya kastaafu
kwamaana huko ndiko watakapo pata uzoefu wakutosha kabla ya ile miak
55 mnayoihitaji ninyi” alisema Ghasia.
Alisema LAPF wanatakiwa kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa fao la
elimu haraka iwezekanavyo,kwani ameshataarifiwa kuwa fao hili limeanza
kushughulikiwa kuanzia mwaka jana.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo ambao ni wa siku
mbili Mwenyekiti wa bodi ya LAPF Profesa Hassa Mlawa,alisema LAPF
tangu  mwaka 2009/10 ukifanya vizuri kwa kupata hati safi zaidi ya
miaka mitano na katika kipindi cha miaka mine mfuko umepewa tuzo ya na
bodi ya wakaguzi na wahasibu (NBAA).
Naye mkurugenzi mkuu wa LAPF Elihudi Sanga alisema mfuko huo katika
mwaka wa fedha 2012/2013 mfuko huo uliandikisha wanachama takribani
17,840 ikilinganishwa na wanachama 12,466 walioandikishwa mwaka
2011/2012 ambapo katika mwaka wa fedha 2013/2014 wanatarajia
kuandikisha wanachama wapya 20,000 toka sekta zote za kiuchumi.
Mkutano huo utajadili changamoto mbali,kubadilishana mawazo na njia
mbalimbali za kuboresha ,huku kauli mbiu ya mwaka huu ikisema, kukidhi
kwa mafao ya wastaafu ,changamoto na njia za kuboresha.

Post a Comment

أحدث أقدم