Mwanzo mbaya kwenye msimu wa Manchester United umeendelea tena hii leo baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi kuu ya England kulazimishwa sare ya 1-1 na Southampton katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford .
United walianza kupata bao likifungwa na Robin Van Persie ambaye alipata pasi iliyoanzishwa na kiungo Adnan Januzaj lakini mwishoni kabisa mwa mchezo beki wa kimataifa wa Croatia Dejan Lovren aliisawazishia Southampton .
Katika michezo mingine Liverpool na Newcastle United walitoka sare ya 2-2 . Newcastle walianza kufunga kupitia kwa Johan Cabaye kabla ya Steven Gerrard hajaisawazishia Liverpool kwa Penalty . Newcastle walifunga bao la pili kupitia kwa Paul Dummett lakini Daniel Sturridge aliisawazishia Liverpool.
Arsenal waliwafunga Norwich City 4-1 , Chelsea wakawafunga Cardiff City kwa idadi kama hiyo ya 4-1 ,Swansea City nao wakaendeleza mfululizo wa matokeo ya ushindi wa mabao manne wakiwafunga Sunderland 4-0 ,Everton wakashinda mchezo wao dhidi ya Hull City kwa matokeo ya 2-1 na Stoke City na West Bromwich Albion wakatoka sare ya bila kufungana .
No comments:
Post a Comment