Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano na Katibu Mkuu wa EAC,Dk Richard Sezibera leo
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Balozi Dk Richard Sezibera amesema mgogoro kati ya Rais wa Tanzania,Dk Jakaya Mrisho Kikwete na mwenzake wa Rwanda,Paul Kagame hauwezi kuathiri kwa kiwango cha kuvunja jumuiya hiyo japo sio afya kwa juhudi za mtangamano.
Amesema jitihada za kuutatua mgogoro zinafanywa na EAC pasipo kutaka kuingiliwa na vyombo vya habari na kua njia pekee ya kuumaliza ni kwanjia ya kidiplomasia.
"Tunaendelea na mashauriano ambayo hatujapenda vyombo vya habari kuingilia kwa sasa,tunaamini njia sahihi ni njia ya kidiplomasia zaidi"
Hata hivyo alikanusha taarifa zilizoenea kuwa wafanyakazi wa Tanzania na Rwanda wanaofanya kazi EAC wamekuwa hawasemeshani kutokana na mgogoro huo.
Dr Sezibera akizungumzia raia wa kigeni walioamriwa kuondoka mkoani Kagera ,alisema anaamini kila nchi ina utaratibu wake lakini hakuna sababu ya kuwaita raia wa Afrika Mashariki wahamiaji haramu kwani wananchi wa eneo hili ni wamoja.
Alisema Kanda ya Afrika Mashariki inakabiliwa na migogoro mikubwa ukilinganisha na maeneo mengine yakiwamo makundi yaliyofanya mauji ya kimbali na mengine kama kikundi cha FNL cha Burundi na mengine jambo linalohatarisha usalama kwa ujumla.
|
No comments:
Post a Comment