June 18, 2013
BREAKING NEWS:HALI NI TETE KWA SASA ARUSHA,MABOMU YA MACHOZI NA VISHINDO YAPIGWA KUSAMBARATISHA UMATI
Wananchi hata hivyo walijikusanya kuwasubiri viongozi wa Chadema
Mabomu ya machozi yaliporindima kila mtu alitafuta njia yake kujinusuru
Hata viatu vilisahaulika ili mradi tu kujiokoa na kadhia hiyo
Jamaa akinawa uso baada ya kuzidiwa na mabomu ya machozi
HALI tete katika jijini la Arusha muda huu,Polisi wanapiga mabomu ovyo,watu waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Soweto wakisubiri kuaga miili ya watu waliopoteza maisha katika shambulio la kigaidi wametawanywa kwa mabomu.
Hatua hiyo imewafanya wananchi kukimbia hovyo huku wengine wakipoteza vitu mbalimbali kama viatu,saa,simu na mikoba wakati wakijaribu kuokoa maisha yao.
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao,Freeman Mbowe kila mmoja alikua akitafuta njia yake kujiokoa na habari ambazo hajithibitishwa zinasema Mbowe na Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu wametiwa mbaroni.
Mabomu ya machozi na vishindo yanaendelea kusikika kila kona ya jiji la Arusha lengo likiwa kusambaratisha vikundi vidogovidogo na kurejesha hali ya amani.
Katika maeneo mbalimbali hasa eneo la makutano ya soko la Ngarenaro na Shoprite hali ya magari ilikuwa mbaya kutokana na foleni iliyochangiwa na madereva kukimbia mabomu hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment