Mbunge wa Ubungo ambaye ni Mkurugenzi wa Habari wa Chadema
Pamoja na kuwa wana
ushahidi wa Picha, Mikanda ya Video inayoonyesha jinsi Polisi walivyoshiriki
kulipua bomu la Arusha, Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wamesema
hawapo tayari kupokea pesa zilizotengwa na serikali kwa ajili ya mtu atakayetoa
taarifa kuhusu waliohusika na mlipuko wa
Arusha.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari Ofisi za Chama hicho Makao Makuu, Msemaji wa Chama hicho, John Mnyika
ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo alisema “hata kama bado hatujakaa kama Chama
kuafikiana suala hili, hizo pesa kuzichukua ni ufisadi tu, matumizi mabaya ya
pesa, serikali imepata wapi pesa za kulipa milioni mia kwa watoa taarifa wakati
haijawahi hata kutoa rambirambi kwa mjane wa Daudi Mwangosi, licha ya kwamba
Polisi walihusika kwa asilimia zote katika kuua, hatuwezi kuhuchukua hizo
pesa.
Kwanza ifahamike kwamba
serikali imeamua kutenga hilo fungu ili kuhalalisha matumi mabovu ili
kuhalalisha ulaji wa pesa, ije iseme tuliwalipa watoa taarifa, huu ni uongo, na
serikali inapokuwa inadanganya raia wake inakosa uadilifu wa kuendelea kutawala.
Suala la Arusha ni tete,
serikali imekuwa ikisema uongo hapa na pale, ndio maana hata Mizengo Pinda tangu
aseme uongo suala hilo halijawahi kuzungumzwa Bungeni, Spika analipiga danadana
kila mara.
Chanzo:Emmanuel Shilatu
No comments:
Post a Comment