AIR UGANDA KUTUA KIA
Arusha
Shirika la ndege la Uganda (Air Uganda)
limeongeza KIA kuwa kituo kipya katika vituo saba ilivyokua navyo awali na
kuonesha hatua kubwa iliyopigwa na shirika hilo lililo na makazi yake Entebe
Uganda, katika sekta ya soko lake Africa
Mashariki.
Baada ya kutua
kwa mara ya kwanza ndege hiyo yenye namba U7331 iliyokua imebeba abiria wapatao
19 wakiwemo viongozi wa shirika hilo na baadhi ya watalii katika uwanja wa
kimataifa wa Kilimanjaro, uzinduzi huo ulifuatiwa na hafla fupi iliyowaweka
wadau pamoja.
Akizungumza
katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa KADCO bwana Bakari Murusuri
alisema “Ni furaha kubwa kuwakaribisha ‘Air Uganda’ katika kiwanja chetu cha
kimataifa cha KIA. Tunaamini kuwa shirika hili litafurahia huduma zetu hapa KIA
kwani wamechagua eneo sahihi lilozungukwa na fursa nyingi kiuchumi kama Utalii”
Akiushukuru uongozi
wa KADCO kwa mapokezi mazuri na ushirikiano waliouonyesha katika uzinduzi wa
safari mpya ya Kilimanjaro Mkurugenzi mtendaji wa Air Uganda Cornwell Muleya ameahidi
kutoa ushirikiano wa hali na mali na kusema kuwa hii ni fursa kubwa ya kukuza uchumi wa Tanzania
kupitia Utalii.
Nae Meneja
Maendeleo ya kibiashara Bi Christine Mwakatobe alisema...... “Tunajivunia
kuongeza mashirika ya ndege ya kimataifa kutua hapa KIA moja kwa moja kutoka katika
nchi zao. Mwaka jana tulipokea mashirika mbalimbali kama Kenya Airways, Qatar
Airways, na Turkish Airlines na hii inathibitisha juhudi za makusudi tunazozifanya
kupanua wigo wa soko letu”. Aliongeza kwa kusema “mbali na mashirika
yanayofanya safari zake ndani ya nchi kutoka kiwanja cha kimataifa cha
Kilimanjaro yanayosimamiwa na KADCO, mashirika mengine ya kimataifa ni pamoja
na KLM, Ethiopian Airlines, Emirates, Turkish Airlines, Kenya Airways, Qatar
Airlines.”
Air Uganda
itafanya safari zake mara nne kwa wiki na ndege nambari CRJ-200 katika ruti
ya Entebbe – Kilimanjaro – Mombasa.
No comments:
Post a Comment