Pages

May 6, 2013

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AMEFIKA KATIKA KANISA KATOLIKI LA MT.JOSEPH MFANYAKAZI,PAROKIA YA OLASITI,JIMBO KUU LA ARUSHA KUWAFAJIRI WAFIWA NA MAJERUHI



Na Mwandishi wetu,Arusha
Taasisi ya ujasusi ya Marekani(FBI)wameingia jijini Arusha kuchunguza tukio la ulipuaji wa Kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Parokia ya Olasiti jijini Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameyasema hayo jioni ya leo wakati akitoa taarifa kwa waziri Mkuu,Mizengo Pinda aliyefika kuwafariji wafiwa na kutoa tamko la serikali

Pinda amesema kuwa hakuna mtu atakayeweza kukomesha dini nyingine kwa kuua viongozi wa dini yeyote bali jambo linalitakiwa ni kuvumiliana watu wa imani tofauti na kuendelea kudumisha amani

Watu mbalimbali wanashikiliwa wakiwemo raia wanne wa Saudia Arabia ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA)na kuondoka nchini kupitia mpaka wa Namanga wakielekea nchini Kenya baada ya tukio kutokea.
Paroko wa Kanisa Katoliki,Parokia ya Olasiti,Padri Peddy Costelino akitoa maelezo jinsi mlipuko ulivyotokea jana(katikati) ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais(Mahusiano)Stephen Wasira na Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsikiliza Msaidizi wa Askofu Jimbo Kuu la Arusha,Simon Tenges

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akilakiwa na Paroko wa Kanisa Katoliki,Parokia ya Olasiti,Padri Peddy Costelino

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi

Paroko wa Kanisa Katoliki,Parokia ya Olasiti,Padri Peddy Costelino akizungumza

Paroko wa Kanisa Katoliki,Parokia ya Olasiti,Padri Peddy Costelino akizungumza

Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowassa akizungumza leo
Waziri wa nchi ofisi ya Rais(Mahusiano na Uratibu)akitoa salamu za pole

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akitoa salamu zake

Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Arusha,Catherine Magige akitoa salamu zake

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa salamu za serikali kwa kuwataka wananchi kutoa taarifa zitakozoweza kuwatia mbaroni wahalifu
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri Mkuu,Pinda wakiwa kwenye eneo la kanisa liliopotokea tukio la maafa ya mabomu

Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...