Pages

May 10, 2013

ANGELA MERKEL AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA NCHINI AFGHANISTAN.

Merkel nchini AfghanistanKANSELA Angela Merkel wa Ujerumani leo Ijumaa amefanya ziara ya ghafla kaskazini mwa Afghanistan kuvitembelea vikosi vya nchi yake siku sita baada ya kuuwawa kwa mwanajeshi wa kikosi maalum cha Ujerumani. 
Msemaji wa kijeshi Luteni Kanali Marco Schmidt amesema Kansela Angela Merkel amewasili katika mji wa Mazar-e-Sharif wakati wa asubuhi leo hii ambapo alikuwa akitegemewa kuwepo kwa masaa machache tu. 

Msemaji huyo kwa sababu za kiusalama amekataa kutowa maelezo zaidi ila amesema kwamba hakuna mipango kwa Merkel kukutana na Rais Hamid Karzai au kuz
ungumza na rais huyo wa Afghanistan kwa njia ya simu.Katika ziara yake hiyo Merkel ameandamana na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Thomas de Maiziere.

Hapo tarehe 4 mwezi wa Mei waasi waliokuwa wakivurumisha maroketi wamemuuwa mwanajeshi mmoja wa Ujerumani na kumjeruhi mwengine katika jimbo la kaskazini la Baghlan. 

Hiyo ni mara ya kwanza kutokea kwa kifo cha mwanajeshi wa kikosi maalum cha Ujerumani kilioko Afghanistan.

Kikosi hicho kinahesabiwa kuwa na ujuzi mkubwa ni kama kile cha Marekani kinachojulikana kwa jina la Navy SEAL ambapo wakati huo kilikuwa kikiongoza operesheni za kijeshi nchini Afghanistan.

Wanajeshi wa Ujerumani 35 wameuwawa nchini Afghanistan tokea mwaka 2002.

Ujerumani ina vikosi vingi.
Kansela Angela Merkel na Waziri wake wa Ulinzi Thomas de Maiziere wakitembelea vikosi vya Ujerumani vilioko Kundus. (10.05.2012) Kansela Angela Merkel na Waziri wake wa Ulinzi Thomas de Maiziere wakitembelea vikosi vya Ujerumani vilioko Kundus. 
 
Ikiwa na zaidi ya wanajeshi 4,000 waliowekwa nchini Afghanistan Ujerumani ni nchi ya tatu yenye wanajeshi wengi katika kikosi cha kimataifa kilioko Afghanistan na imeahidi kubakisha wanajeshi 800 nchini humo baada ya operesheni ya mapambano ya NATO kumalizika mwishoni mwa mwaka 2014.

Marekani inatarajiwa kubakisha wanajeshi 10,000 nchini Afghanistan baada ya mwaka 2014 lakini bado haukufikiwa uamuzi rasmi juu ya suala hilo.

Vikosi vya Ujerumani vitaendelea kubakia hadi hapo mwaka 2017 kwa ajili ya kutowa mafunzo,ushauri na msaada kwa vikosi vya usalama vya Afghanistan na vitawekwa katika mji mkuu wa Kabul na Mazar-e-Sharif. 

Baada ya mwaka 2017 Ujerumani imesema itakuwa tayari kuchangia wanajeshi 200 hadi 300.

Sharti la kubakisha vikosi.
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan. Rais Hamid Karzai wa Afghanistan.
 
Uamuzi wa mwisho kuhusu vikosi vya Ujerumani vitakavowekwa nchini Afghanistan baada ya mwaka 2014 utatolewa na serikali mpya baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika hapo mwezi wa Septemba ambapo kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni Merkel anatarajiwa kushinda muhula wa tatu wa kipindi cha miaka mingine minne madarakani. 

Wakati mpango huo wa kuwekwa kwa vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan kwa kiasi kikubwa haungwi mkono na wananchi, unaungwa mkono na vyama vikuu vya kisiasa.

Suala la Ujerumani kuendelea kuweka vikosi vyake nchini Afghanistan pia linahitaji ombi la serikali ya nchi hiyo.

Katika hafla iliofanyika katika mji mkuu wa Kabul hapo Alhamisi,Rais Hamid Karzai amesema alikuwa anataka kila nchi mwanachama wa nchi 28 za Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuzungumza moja kwa moja na serikali yake juu ya idadi ya wanajeshi inaotaka kuwaweka nchini humo,mahala pa kuwaweka na vipi vikosi hivyo vitakvyoweza kuinufaisha nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...