Filbert
Rweyemamu,Arusha
Miili ya
waumini wa kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti,Jimbo
Kuu la Arusha imezikwa leo na kugubikwa na majonzi makubwa.
Vilio
vilitawala baada ya wasifu wa marehemu kusomwa hasa wa Patricia Joachim Assey
aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Elerai na kumuona
Pacha mwenzake Patrce akilia sana.
Pia
mwanafunzi mwingine James Gabriel Kessy aliyekua anasoma kidato cha tatu katika
Shule ya Sekondari Arusha Day alisababisha kilio kikubwa kwa waombolezaji.
Katika hatua
nyingine Mwadhama Polycap Kadinali Pengo aliwataka wakristo kutolipiza ubaya
kwa ubaya bali wema kwa ubaya kama maandiko matakatifu yanavyosema na kuwa kwa
kusema hivyo haimanishi serikali iache wajibu wake wa kulinda watu na mali zao
na kutokomeza ugaidi.
Viongozi
mbalimbali waliohudhuria mazishi hayo pamoja na maaskofu wa madhehebu
mbalimbali,viongozi wa serikali wakiongozwa na waziri Mkuu Mizengo Pinda,Waziri
wa Mambo ya Ndani,Dk Emmanuel Nchimbi,Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Makazi,Godluck Ole Medeye na Naibu Waziri wa Tamisemi,Agrey Mwandry.
No comments:
Post a Comment