
Pichani
ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Mizengo
Kayanza Peter Pinda (wa Kwanza Kushoto) akiwa pamoja na Mbunge wa
Simanjiro, Bwana Christopher Ole Sendeka (Wa pili kushoto), Aliyekuwa
Mkuu wa Mikoa Mbalimbali hapa Nchini, Bwana Ditopile Ukiwaona Mzuzuri
(wa tatu kushoto) na wa mwanzo upande wa kulia ni Kijana wa Mjini
William Vangimembe Lukuvi.Picha hii ilipigwa Miaka ya 80 wakati huo Vijana hawa wakiwa ni Viongozi wa Jumuia ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete
akionekana katika Sare zake za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).Picha hii inatajwa kupigwa Mwanzoni mwa Miaka ya 80 wakati huo Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Jeshini.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anne Simamba Makinda
katika Kivazi chake na Namna alivyotengeneza nywele zake.Picha hii ilipigwa Mwaka 1994 wakati Mama Anne Semamba Makinda akiwa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.
Gavana
wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, Waziri wa Zamani wa Fedha,
Mfanyabiashara na Mkulima Mashuhuri, Mchunga Mbuzi aliyebobea, Fundi
Viatu aliyepata Elimu kwa Msaada wa Chama cha Ushirika, Mwasisi wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na Mmoja wa Viongozi
Madhubuti wa Taifa hili, Mzee Edwin Mtei.Picha hii ilipigwa Mwezi Aprili Mwaka 1974 wakati Bwana Edwin Mtei alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini Maarufu zaidi kama "Rais wa Mbeya",
Mwanaharakati wa Utetezi wa Haki za Wanamuziki na Mwanamuziki Mkongwe
wa Muziki wa Kughani wa Kitanzania Bwana Joseph Mbilinyi "Mr 2/Too
Proud/Sugu" (Katikati mwenye Kofia) akiwa na Maswahiba zake miaka
kadhaa Nyuma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamaoja na Mwadhama Kardinali Laurean Rugambwa, Picha hii ilipigwa katikati ya miaka ya 90.

Bibi
Titi Mohammed. Hii ilipigwa Mwaka 1957 wakati Bibi Titi Mohammed akiwa
anahutubia Wananchi katika moja ya mikutano ya Chama cha TANU.

Waziri Mkuu wa Zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr, Salim Ahmed Salim.Picha
hii ilipigwa Mwaka 1970 wakati Dr. Salim Ahmed Salim akiwa katika Ofisi
ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kujitambulisha kama Balozi Mpya
Mteule wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Mbaraka
Mwinshehe Mwaruka japo Vijana wenzie wa Zamani walipenda kumuita majina
Mbalimbali kulingana na Umahiri wake katika Kutunga, kuimba na Kupiga
Gitaa akiwa katika Bendi ya Morogoro Jazz mpaka alipounda Bendi yake ya
Super Volcano.
Haijalishi ulizaliwa enzi za uhai wake au baada
ya kifo chake, jambo moja ambalo wote tunafanana ni kwamba ukisikia
muziki wake sio ajabu utatikisa kichwa, kutabasamu, kucheza au kurukaruka.
Alifariki
kwa ajali ya gari Nchini Kenya tarehe 13 Januari mwaka 1979, kifo chake
kikichangiwa zaidi na kuvuja damu nyingi na asipatikane wa kumchangia
damu ili kuokoa maisha yake pale hospitalini Mombasa.
Pichani ni Mbaraka Mwinshehe akimvisha Pete ya Ndoa mke wake, Amney Shadad, Hiyo ilikuwa tarehe 17/3/1972 Mjini Morogoro.

Aliyekuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye mazungumzo na Mfalme wa Muziki wa Pop Duniani na Mwanamuziki Mashuhuri
wa Marekani, Marehemu Michael Joseph Jackson Ikulu Jijini Dar es
salaam. Picha hii ilipigwa Mwaka 1992 wakati Mfalme huyu wa muziki wa
Pop wa Marekani, hayati Michael Jackson alipoitembelea Tanzania na
kufanya Kitendo cha Kiungwana kwa kufika katika Shule Maalum ya Watoto
Yatima na wenye Mtindio wa Ubongo iliyopo Sinza, Jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani hadi anakufa 2009,
alifika nchini akiwa Balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa
kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Balozi Ahmed
Hassan Diria.

Meya
wa wa Kwanza Mweusi wa Jiji la Dar es salaam, sheikh Amri Abedi Kaluta
(wa Nne Kulia) akimtambulisha Mume wa Malikia waUingereza ambaye pia ni
Bwana Jumbe wa Edinburg (Duke of Edinburg) Prince Philip (wa Pili kulia
Mwenye Sare za Jeshi) kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania na
Kardinali wa Kwanza Mwafrika Duniani, Mwadhama Laurean Rugambwa (wa
Kwanza kulia). Pamoja na Kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam Sheikh Amri
Abedi Kaluta pia alikuwa Kiongozi Mkubwa wa Kidini wa Waislam hapa
Nchini Tanzania.
Credits: Jamii Forum
إرسال تعليق