• Kima
cha chini sasa 200,000/-
Dodoma
|
WAKATI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani,
amekataa kutaja nyongeza ya mishahara ya kima cha chini kwa madai kuwa ni
siri, imebainika kuwa mishahara hiyo imeongezeka kwa sh 30,000 tu.
Nyongeza
hiyo inafanya kima cha chini cha mishahara ya watumishi wa umma, kufikia sh
200,000 kutoka sh 170,000 za mwaka wa fedha uliopita 2012/2013.
Baadhi
ya wabunge walio kwenye Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala
iliyokuwa ikijadili kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, waliliambia gazeti hili kuwa kima cha chini cha mshahara
kimeongezeka kwa sh 30,000.
Hata
hivyo, wakati akifanya majumuisho ya wizara yake jana, Waziri Kombani licha
ya baadhi ya wabunge kumtaka atangaze kiwango kilichoongozeka, alisema kuwa
hawezi kufanya hivyo kwani mshahara wa mtu ni siri.
“Kuhusu
masilahi ya watumishi wa umma. “Hapa msinilazimishe kima cha chini, hapana.
Hata sisi wabunge tunapoona kwenye magazeti yakitangaza mishahara yetu,
hatufurahi kwa sababu mshahara ni siri yako,” alisema Kombani.
Waziri
alirejea kauli yake juzi wakati akiwasilisha mwelekeo wa bajeti ya wizara
yake kwamba kwa mwaka wa fedha 2013/2014 serikali imetenga sh trilioni 4.7.
Kiasi
hicho ni kwa ajili ya nyongeza ya mishahara na kugharamia mishahara kwa
watumishi wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Wakala wa Taasisi za
Serikali.
Kwa
mujibu wa Waziri Kombani, kiasi hiki cha sh trilioni 4.7, pia kitatumika
kugharamia ajira mpya 61,915, upandishwaji vyeo na nyongeza za kawaida za
mishahara za mwaka, pamoja na nyongeza za mishahara kuanzia Juni 2013.
Mwaka
wa fedha uliopita 2011/12, serikali ilitenga sh trilioni 3.7 ambapo mshahara
wa kima cha chini uliongezeka kwa sh 20,000 na kufanya kima cha chini kupanda
kutoka sh 150,000 hadi sh 170,000.
Hata
hivyo Waziri Kombani aliwataka watumishi kuwajibika kwani wapo wanaolalamikia
kutaka nyongeza ya mishahara, lakini hawataki kuwajibika.
Waziri
Kombani alisema serikali imeandaa operesheni maalumu ya kufanya uhakiki wa
vyeti vya watumishi wote nchini ili kubaini walioingia kazini kwa kutumia
vyeti vya kughushi.
Alisema
wapo baadhi ya waliotumia vyeti vya marehemu na wengine ndugu zao ambao pia
wameajiriwa katika majina mawili ya watu wanaofanana.
Wakati
serikali ikiongeza mishahara kwa kiwango kidogo, Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (TUCTA), limekuwa likipendekeza kima cha chini kiwe sh 300,000 na
katika mwaka huu wa fedha, imependekeza kima cha chini kiwe sh 400,000 ili
kukabiliana na gharama za maisha zilizoongezeka mara dufu.
|
No comments:
Post a Comment