• Mbowe
ambana Spika aeleze kanuni iliyotumika
Dodoma
|
WAKATI
wabunge sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakianza
kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge la Bajeti
vinavyoendelea mjini hapa, utata mkubwa umeibuka juu ya kanuni alizotumia
Naibu Spika, Job Ndugai, kutoa adhabu hiyo.
Utata
huo ulibainika jana wakati Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman
Mbowe, alipoomba mwongozo wa Spika Anna Makinda, kutaka kujua kanuni
aliyotumia Ndugai wakati hakuna kanuni iliyomruhusu kutoa adhabu hiyo.
Baadhi
ya wabunge waliozungumza na gazeti hili jana pia walihoji kifungu
kilichotumika hata kama wabunge hao walikosea.
Miongoni
mwa waliohoji adhabu hiyo, wapo baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawakupenda
kutaja majina yao, wakisema kuwa uamuzi wa Naibu Spika ulitawaliwa na jazba
za kibinadamu badala ya kufuata kanuni zinazoliongoza Bunge.
Katika
mwongozo wake jana kwa Spika Makinda, kiongozi huyo wa kambi ya upinzani alihoji
kifungu kilichotumika kuwaadhibu wabunge wake.
Mbowe
alisema juzi wakati Bunge lilipokuwa katika kipindi chake cha jioni, wabunge
sita wa CHADEMA waliotolewa nje kwa maelekezo ya Naibu Spika, Job Ndugai.
Aliwataja
wabunge waliotolewa kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Haghness Kiwia
(Ilemela), Ezekia Wenje (Nyamagana), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph
Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Pete Msingwa (Iringa Mjini).
“Na
wabunge hawa walipotolewa, walipewa vile vile adhabu ya kutohudhuria vikao
vitano vya Bunge, adhabu iliyotolewa papo kwa papo na Naibu Spika.
“Kwa
mujibu wa kanuni zetu, kanuni inayompa Naibu Spika au Spika mamlaka ya kumtoa
mbunge kwa siku tano ni kanuni ya 73 ya kanuni ndogo ya tatu ambayo inahusu
mbunge ambaye atashindwa kutoa vielelezo vya aidha kusema uongo ambayo
inasema hivi: “Endapo mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha maneno aliyoyasema
na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, ameshindwa kutoa uthibitisho huo,
Spika anaweza kumsimamisha mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi
vitano,” alinukuu.
Mbowe
ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA, alisema yaliyotokea bungeni juzi ni
sintofahamu kati ya wabunge na kiti cha Spika ambapo katika mambo ya msingi
CHADEMA ilitegemea kifungu cha nne cha kanuni za Bunge, kifungu kidogo cha kwanza
kingetumika.
Kifungu
kinasema: “Spika anaweza kutaja jina la mbunge kwamba amedharau mamlaka ya
Spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge.
“Ikiwa kwa
maneno au vitendo, mbunge huyo anaonyesha dharau kwa Spika au atafanya
kitendo chochote cha makusudi cha kudharau shughuli ya Bunge au mbunge yeyote
anayeongoza shughuli hiyo.”
Kutokana
na kanuni hiyo, Mbowe aliomba mwongozo wa Spika kutaka kujua wabunge
hao walitolewa kwa kanuni gani na ni lini wataweza kurejeshewa haki yao
ya kurejea ndani ya Bunge.
Vituko
vya juzi
Baadhi
ya askari walioamriwa kuingia ndani ya Bunge, walisema hawakuwa tayari kumtoa
Lissu kwa nguvu ndio maana walitumia muda mrefu kutimiza agizo hilo.
Askari
hao walisema hofu yao ilikuwa ni usalama wa Waziri Mkuu kwani endapo vurugu
zingeibuka, angekuwa katika wakati mgumu kiusalama.
Baada
ya Lissu na wabunge wenzake kutoka nje ya ukumbi chini ya ulinzi, askari hao
walipata wakati mgumu kuwatoa nje ya eneo la Bunge.
“Tulipanda
juu hadi kwenye ofisi ya Lissu, alipofika alikaa chini, akafungua kompyuta
yake, baadaye akaizima wala hakuwa na haraka na sisi wakati huo tulibaki
tumesimama tu.
“Baadaye
aliizima, akachomoa waya na kuziingiza kwenye begi lake, kisha
alisimama taratibu na kuondoka kama vile hakuna jambo lililotokea,” alisema
askari huyo.
Wenyewe
wanena
Lema
alisema: “Nimepokea kwa furaha adhabu hii kwa sababu imetokana na kupigania
haki na ukweli ndani ya Bunge. Kwa hiyo adhabu hii kwangu ni baraka.”
Alisema
uonevu wa wazi uliofanywa na Naibu Spika, Job Ndugai, baada ya muda kidogo
Tanzania itashangilia ushindi mkubwa. Kwamba Watanzania watafurahia vijana
wao na watoto wao walioshinda hofu.
“Ushahidi
nilioombwa kuhusu mwenyekiti wa CCM kuwa mwasisi wa udini ninao, tena wa
uhakika wa nguvu na imara na niko tayari kuutoa mbele ya Bunge kwa kuwa
nilitoa maneno hayo mbele ya Bunge.
“Sitapeleka
tena ushahidi wangu vichochoroni kwa kuwa nilipeleka ushahidi wangu kwa Spika
kuhusu uongo wa Waziri Mkuu, walipiga chenga hadi wakanivua ubunge,” alisema.
Lema alidai
kuwa ametumiwa meseji za vitisho kwamba wangelimuonyesha tena mahakamani,
lakini akasema wafanye wafanyavyo ila moyo wake una furaha kuwa amesema yale
ambayo wengine wameogopa kuyasema.
Mbunge
wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, alisema: “Bunge letu lina matatizo, halina
mwelekeo. Job Ndugai anajidai yeye ndiye kiongozi wa serikali.”
Alisema
kama Ndugai ana sifa hizo na anajiandaa kuwa Spika wa Bunge lijalo, anamwomba
Mungu asiwe mbunge katika Bunge hilo.
“Tusi
lililotolewa na Peter Serukamba wa CCM, lilikuwa kubwa kuliko matusi yote
yaliyowahi kutolewa ndani ya Bunge katika mabunge ya Jumuiya ya Madola.
“Hili
lilihitaji adhabu, lakini kitendo cha Naibu Spika kumtimua Lissu ambaye
alikuwa anafuata kanuni ni cha kusikitisha sana,” alisema.
Mbilinyi
alisema wananchi wa Mbeya Mjini hawakumtuma kushangilia bungeni.
Kwa
upande wake Mchungaji Msigwa alisema: “Adhabu hii ni ya hovyo kwa sababu
haikufuata taratibu; wamegeuza Bunge kama sehemu ya serikali.”
Alifafanua
kuwa kama angepata adhabu iliyofuata kanuni asingekuwa na shida, angeipokea
kwa furaha.
“Naibu
Spika ana jazba, anapaswa apate mafunzo ya jazba zake. Viongozi wa Bunge
wamejaa u-CCM zaidi kuliko utaifa. Binafsi sitajali kufukuzwa, ninachotaka
haki itendeke,” alisema.
Mbunge
wa Ilemela, Kiwia, alisema adhabu waliyopewa ni kinyume cha kanuni.
“Adhabu
hiyo anapaswa apewe mtu aliyesema uongo na kushindwa kuthibitishwa, pamoja na
hayo kanuni zifanye kazi kwa wabunge kwa usawa,” alisema.
Kiwia
aliongeza kuwa kanuni hazipaswi kuwaona wabunge wengine wana haki na wengine
hawana; kwamba hoja za msingi zijibiwe, maamuzi bungeni yasifanyike kwa
mabavu.
Naye
Lissu ambaye ni mwanasheria kitaaaluma, alisema hajui ni kanuni gani
iliyotumika na kumwadhibu na kwa kosa gani.
|
No comments:
Post a Comment