Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha(APC)kitafanya mkutano wake wa mwaka ambao utawachangua viongozi wapya kushika nyazifa mbalimbali za uongozi wa chama hicho.
Akizungumza mapema leo kwenye kikao cha dharula kilichokuwa na lengo ya kupanga siku ya uchaguzi ambayo imekubaliwa kuwa ni Juni Mosi,mwaka huu,Mwenyekiti wa APC,Claud Gwandu alisema ameita kikao hicho ili kuomba ridhaa ya wananchama kupanga tarehe ya mkutano mkuu na uchaguzi kutokana na kukabiliwa na maandalizi ya siku ya vyombo vya habari itakayofanyika katika ngazi ya Kanda kwenye jiji la Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 200.
Alisema kikatiba uchaguzi ulitakiwa kufanyika mwezi Mei lakini kutokana na kuwa APC ndio wenyeji wa siku ya vyombo vya habari imeonekana ni busara kusogeza mbele siku ya mkutano mkuu ambayo itaenda sanjari na kufanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa APC.
Kikao hicho kimewapitisha wajumbe watano watakaosimamia uchaguzi huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na kila mwanachama kuamini ana uwezo wa kuongoza akishirikiana na wanachama wenzake.
Katibu wa APC,Eliya Mbonea alisema mchakato wa kuandaa fomu zitakazotumwa kwa wanachama utafanywa na kamati ya uchaguzi ambayo wajumbe wake ni waandishi wakongwe,Willam Lobulu,Danford Mpumilwa,Mch Amos Sekajingo,Zephania Ubwani na Kulwa Mayombi.
Baadhi ya wanachama waliozungumza na Blog hii hawakupenda kutaja nafasi watakazowania kuwa ni mapema mno kutangaza na ni moja ya mbinu za kisayansi kusaka ushindi.
Uongozi unaomaliza muda wake unajivunia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kuwa na ofisi ya kudumu,mafunzo ya mara kwa mara,vitendea kazi na baadhi ya wanachama kulipa ada kwa wakati.
Mwandishi Chipukizi na Mkurugenzi wa BIMO,Bertha Mollel akisalimiana na waandishi wakongwe,Charles Ole Ngereza na Antony Masai |
David Frank akiperuzi kurasa za gazeti la Mwananchi Jumamosi |
Taswira za leo |
Popote ulipo habari lazima ziufikie ulimwengu,si mwingine ni Veronica Mhata wa Habari Leo(katikati)akiwa na Mustafa Leu wa Radio Uhuru(kushoto) na Cynthia Mwilolezi wa gazeti la Nipashe |
Viburudisho virikuwepo vya kutosha |
Makamu Mwenyekiti wa APC,Charles Ole Ngereza(kushoto)akielekezana jambo na Veteran Antony Masai wa Tripple A |
Katibu wa APC,Eliya Mbonea(kulia) akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa APC,Charles Ole Ngereza(kushoto)na Mwenyekiti,Claud Gwandu kabla ya kuanza kikao mapema leo |
Katibu wa Arusha Press Club(APC)Eliya Mbone akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wake,Claud Gwandu |
Mwenyekiti wa Arusha Press Club,Claud Gwandu akizungumza |
Kutoka kushoto,Daniel Sabuni(Mwananchi)Cynthia Mwilolezi(Nipashe)na Janeth Mushi wa Jambo Leo |
Veronica Mheta akiula swali.Picha zote na Filbert Rweyemamu |
No comments:
Post a Comment