ARUSHA, TANZANIA.
MBUNGE wa jimbo la Arusha mjini
Godbles Lema ameachiwa kwa dhamana hadi May,29 mwaka huu kesi
hiyo itakapotajwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Wafuasi wa Lema walifaika mahakamani hapo mapema sana huku wakiwa kwenye makundi wakijadili namna ya kumpokea kwa shangwe huku wakiwa na matawi ya miti.
Alifikishwa Mahakamani akiwa kwenye gari aina ya Ballon nyeusi ikisindikizwa na gari ya Polisi waliokuwa wamejihami kwa lolote,baada ya kuteremka alionyesha alama ya chama chake ya vema na kisha kuongozwa na askari kanzu kuingia kwenye chumba cha mahakama.
Baada ya Mbunge huyo aliyejozolea umaarufu mkubwa akiwa ameambatana na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nassari kuachiliwa
huru, umati wa wanachama wa Chadema waliokuwa wamejazana katika Mahakama
hiyo walifanya maandamano makubwa kwenda katika Ofisi za chama hicho
zilizopo maeneo ya Ngarenaro.
Mbunge huyo alisomewa shitaka moja la Uchochezi kuwa siku hiyo kwenye eneo la Freedom Square kwenye Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA)alisema Mkuu wa Mkoa hajui chuo hicho kilipo na alikuja kama anayeenda kwenye Send off na kusema kuwa
‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga .Na kuwa iwapo Mkuu wa mkoa asingefika kwa wakati angeongoza msafara kudai haki zao
No comments:
Post a Comment