Ziwa Duluti: Utalii wa Maombi Wavutiwa, Wawekezaji Watakiwa Kuchangamkia Fursa


Naibu Waziri wa Utalii, Hamad Hassan Chande, ametaja uwepo wa utalii wa maombi katika Hifadhi ya Msitu wa Ziwa Duluti, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,mazingira yake ya asili yana fursa kubwa ya kuendeleza aina mbalimbali za utalii,

Amesema utalii huo ndani ya Hifadhi ya Ziwa hilo unasaidia kukuza imani za watu na kuchangia maendeleo endelevu ya eneo hilo hivyo amewataka wananchi na wadau kuendelea kutunza mazingira na vivutio hivyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwaajili ya maendeleo ya Kitaifa na kukuza uchumi.

Ametoa rai kwa wawekezaji wa ndani na nje kuchangamkia fursa katika eneo hilo, hususan katika miundombinu na huduma za utalii, ili kuongeza idadi ya watalii na mchango wa eneo hilo kwni Ziwa hilo halikauki na ni sababu kubwa ya kivutio huku akisisitiza Jamii kwa kushirikiana na Serikali pamoja na sekta binafsi katika kulilinda eneo hilo la utalii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava, aliwaongoza wajumbe wa Kamati hiyo katika ziara ya kutembelea Hifadhi hiyo kwa lengo la kukagua hali ya uhifadhi, kutathmini fursa za utalii wa ikolojia na kujadili changamoto zinazokabili eneo hilo la Ziwa Duluti

Mzava amepongeza na kuzisihi sekta binafsi kuboresha miundombinu na huduma kuelekea maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 ,Sambamba na kuwa taka Watanzania kutembelea vivutio vilivyopo katika Hifadhi hiyo ya msitu wa ziwa Duluti

Peter Myonga ni Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), amesema kuwa TFS imeendelea kuboresha huduma na miundombinu katika Hifadhi ya Msitu wa Ziwa Duluti, ikiwemo kuongeza maeneo ya malazi ili kuhudumia wageni wengi zaidi.

Myonga aliongeza kuwa hifadhi hiyo ina vivutio mbalimbali, ikiwemo utalii wa , matembezi ya kitalii, shughuli za majini,maombi, mandhari ya Mlima Meru , Kilimanjaro,kuna mnyama Kenge, hivyo amewasihi wananchi kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kukuza utalii wa ndani.




Post a Comment

Previous Post Next Post