Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, viongozi wa dini, pamoja na familia, ndugu, jamaa na wananchi.

Mapema, Rais Dkt. Mwinyi ameungana na familia, ndugu na jamaa katika Sala ya Jeneza iliyofanyika Masjid Ihtiswam, Kizimkazi, kabla ya mwili wa Marehemu Hafidh Ameir Hassan kuzikwa katika makaburi maalum ya Kizimkazi.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametoa mkono wa pole kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, watoto na familia ya Marehemu, na kuwafariji katika kipindi hiki cha majonzi.

Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji’un.