Meneja
wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali akiwasilisha taarifa kwa Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Hayupo
Pichani), kuhusu mapato na matumizi ya bandari hiyo, wakati Waziri huyo
alipotembelea bandari hiyo kukagua maendeleo ya mradi wa gati.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiangalia
eneo ambalo linajengwa maegesho ya kawaida ya mizigo katika bandari ya
Mtwara, alipotembelea bandari hiyo kukagua maendeleo ya miradi
inayotekelezwa katika bandari hiyo.
Muonekano
wa hatua iliyofikiwa ya mradi wa Gati katika bandari ya Mtwara. Gati
hiyo yenye urefu wa mita 300 inatarajiwa kukamilika mwaka 2019 na
upanuzi wake utagharimu kiasi cha shiliingi zaidi ya bilioni 100.
Mhandisi
wa Bandari ya Mtwara, Eng. Twaha Msita ambaye ni (katikati),
akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa (kushoto), ramani ya eneo la mradi wa kuegesha mizigo ya
kawaida, alipokagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika bandari ya
Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini
(TPA), Karim Mattaka.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Nchini (TPA), Eng. Karim Mattaka (kushoto), alipokagua maendeleo ujenzi
wa gati, Mkoani Mtwara.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Dott Services ltd (kushoto),
anaejenga Barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50, alipokagua maendeleo ya
ujenzi wake mkoani Mtwara. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini
(TANROADS) Mkoani Mtwara, Eng Dotto Chacha. Wa pili kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Mtwara mjini Bw. Evod Mmanda.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na
wakazi wa Nanguruwe Mkoani Mtwara alipokagua maendeleo ya ujenzi wa
Barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha Lami.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ametoa miezi
mitatu kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), kuhakikisha
inatatua changamoto zote zinazokwamisha mradi wa ujenzi wa gati mpya.
Prof.
Marawa ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Gati
mpya inayojengwa Mkoani Mtwara kwa ubia wa kampuni mbili za Kichina za
China Railways Major Bridges Engineering Group Co. Ltd (CRMBEG) na China
Railways Construction Engineering Group (CRCEG) na kubaini mapungufu
katika utekelezaji wa mradi huo.
“Hatuwezi
kuendelea kuchelewesha mradi huu muhimu kwa wakazi wa Mtwara, wakati
fedha zipo na mikataba imeshasainiwa, naiagiza TPA kuhakikisha kuwa
inatatua changamoto hizo na kuzitafutia ufumbuzi ndani ya miezi mitatu
ili mradi ukamilike kwa wakati,” amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa miradi inayotekelezwa na Wakandarasi wazawa chini ya usimamizi wa
TPA isimamiwe kwa kuzingatia viwango na muda uliopangwa na kuahidi
kurejea baada ya miezi mitatu kukagua maendeleo ya miradi hiyo.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka
amemuhakikishia Prof. Mbarawa kuwa TPA itasimamia kwa karibu mradi huo
na kuhakikisha mapungufu yote yanafanyiwa kazi kwa wakati.
“Nipende
kukuhakikishia Waziri kuwa TPA tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatatua
changamoto zilizopo na kuanzia wiki ijayo tutaongeza kasi ya kutatua
mapungufu yaliyopo ili mradi huu ukamilike kwa wakati,” amesema Mhandisi
Mattaka.
Kwa
upande wake Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali amesema kuwa kwa
sasa mradi wa ujenzi wa gati namba mbili (2) umefikia asimilia 15 na
utakapokamilika utawezesha Meli kubwa na za kisasa aina ya Panamax
kuhudumiwa katika Bandari ya Mtwara ifikapo mwaka 2019.
Katika
hatua nyingine Profesa Mbarawa amekagua ujenzi wa Barabara ya Mtwara
hadi Mnivata KM 50 na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo
na kuahidi kulipa madai ya Mkandarasi Kampuni ya M/s Dott Services ltd
mapema iwezekanavyo ili mradi huo ukamilike kwa wakati.
‘Nimhakikishie
Mkandarasi kuwa madai yake aliyowasilisha tunajipanga kuyalipa ili kasi
iwe kubwa na mradi huu ukamilike kwa wakati kwa kuwa umesubiriwa na
wananchi wa mkoa wa Mtwara kwa muda mrefu’ Amesisitiza Prof. Mbarawa.
Aidha,
Mkandarsi wa Kampuni ya M/s Dott Services ltd amemhakikishia mhe.
Waziri kuwa watahakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na kwa
viwango kama ilivyoahidiwa.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) , Mkoani
Mtwara, Eng. Dotto John ametanabahisha kuwa wakala umejipanga
kuhakikisha unasimamia barabara hiyo kwa kuhakikisha viwango na ubora
vinazingatiwa na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
Prof. Mbarawa yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya miradi ya Miundombinu ya Barabara na Bandari.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment