Pages

March 5, 2018

MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE YA UJENZI WA MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA

Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Geita Iddi Kassim Iddi,akiendesha Harambee ya umaliziaji wa ujenzi wa madarasa kwenye kanisa la AIC Kalangalala. 
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Geita Iddi Kassim Iddi pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo,Leornad Kiganga Bugomola wakifurahia kwa pamoja wakati wa harambee. 
Mjumbe wa SINODI na Mwenyekiti wa idara ya vijana wa kanisa la AIC Kalangalala wakicheza kwa pamoja wakati wa zoezi la uchangiaji wa harambee ya umaliziaji ujenzi wa madarasa ya watoto. 
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Geita Iddi Kassim Iddi,na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita Leonard Bugomola wakiwa kwenye harambee. 
Mchungaji wa kanisa la AIC Kalangalala John Masanyiwa pamoja na mama wakipandisha ngazi kwaajili ya kwenda kutoa mchango wao. 
Mchungaji Johh Masanyiwa akitoa mchang wake pamoja na mama mchungaji. 






wenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita Leonard Bugomola kibadilishana mawazo na katibu wa UVCCM Mkoa wa Geita. 
MNEC Iddi Kassim akipokea zawadi ya kitenge kutoka kwaya ya vijana Geita. 
Mzee Yohana Madundo akiwa na kuku ambaye alipigwa mnada kwaajili ya kupatikana fedha ambazo zinaelekezwa kwenye ujenzi wa madarasa. 
MC Jonathan Masele akiongoza zoezi la mnada wakati wa harambee ya ujenzi wa madarasa. 
Kikundi cha kusifu na kuabudu. 
Mwenyekiti wa idara ya wanawake kanisa la AIC Kalangalala,Bi,Agnes Kamagi akishukuru kanisa kwa kuweza kujitoa kwenye harambee ya umaliziaji ujenzi wa madarasa ya watoto. 
Mch,John Masanyiwa akisoma kiasi ambacho kimepatikana kwenye harambee hiyo ya kanisa. 
Mch,John Masanyiwa akielezea namna ambavyo ujenzi ulianza mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi mkoani Geita Iddi Kassim. 
Madarasa ambayo yamejengwa kwaajili ya watoto wa kanisa la AIC Kalangalala. 
Mgeni Rasmi pamoja na mchungaji na viongozi wa kanisa la AIC Kalangalala wakikagua baadhi ya majengo ambayo yamekwishakujengwa. 
Mchungaji ,John Masanyiwa akitoa maelezo ya namna ambavyo ujenzi unaendelea Kwasasa.


Na,Joel Maduka,Geita.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Geita Iddi Kassim Iddi,amefanikisha upatikanaji wa kiasi cha shilingi milioni 13.2 ,mifuko ya seruji 70 na mabanti ya kisasa 131 kwaajili ya ujenzi wa madarasa ya watoto kwenye kanisa la AIC Kalangalala Wilayani Geita.

MNEC wa mkoa huo Iddi ameendesha harambee hiyo siku ya leo kwenye ibada ambayo ilikuwa imeandaliwa na idara ya wanawake wa kanisa la AIC Kalangalala kwaajili ya changizo la umaliziaji wa madarasa ya kujifunzia watoto kanisani hapo.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya watoto wa kanisa hilo,Bi Justina Yuda ameeleza mahitaji ya ujenzi wa madarasa ya watoto kwa awamu ya pili yanatarajia kugharimu kiasi cha Tsh 19,185,000 na kwamba fedha hiyo itasaidia kuezeka,kuweka dali kwenye madarasa pamoja na kuweka frame za madirisha ,milango na mageti ya milango.Katika harambee hiyo MNEC Iddi milioni 1 papo hapo,mifuko 20 ya seruji na mabati 13 huku akitumia nafasi hiyo kuendesha harambee ambayo iliweza kusaidia kupatikana kiasi cha sh,milioni 12.2 hivyo kupelekea kupatikana kwa jumla ya kiasi cha sh,milioni 13.2 ambazo zitatumika kujenga madarasa ya kujifunzi watoto.

Akihutubia mamia ya waumini hao Mara baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimia waumini wa kanisa hilo MNEC Iddi aliwasisitiza waumini hao kuendelea kuunga jitihada za uchangiaji wa madarasa pamoja na ujenzi hili kuweza kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwakabili wanafunzi wengi kwa sasa.

Pia amewaomba kundelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya inayooongozwa na kusimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani imejipambanua kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao.

Aliwasihi waumini hao kuiombea serikali ya Rais Magufuli sambamba na wateule na watumishi wake wote ili waendelee kuliongoza Taifa na sekta mbalimbali katika ushirika mwema wakiongozwa na roho mtakatifu kila mmoja kwa imani yake.

Aidha kwa upande wake mchungaji wa kanisa hilo John Masanyiwa alisema kukamilika kwa madarasa hayo matatu yatawasaidia watoto kuweza kujifunza katika vipindi vya ibada na pia kwa upande wa idara ya wanawake yatawasaidia kuwa kama kitega uchumi kwa maana ya kukodisha kwaajili ya shughuli mbali mbali zikiwemo za semina na warsha ambazo zitakuwa zikifanyika.

Pia,Mch Masanyiwa amemshukuru MNEC wa mkoa wa Geita kwa kufanikisha shughuli ya harambee hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...