Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa Mkutano
wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa
(TALGWU) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Rayal Village Dodoma
Februari 01, 2018.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano
wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali za Mitaa uliofanyika Dodoma.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.
Erick Shitindi akionesha ishara ya umoja na mshikamano wakati wa Mkutano
wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa
(TALGWU) uliofanyika Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi
wa Serikali za Mitaa (TALGWU) wakifuatilia ujumbe kutoka kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) aliowasilisha
katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Bw. Suleiman
Kikingo akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la
chama hicho uliofanyika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa uliofanyika Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema
kupitishwa kwa muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii utasaidia
kuwanufaisha watumishi wa umma kwa kurahisisha utoaji wa huduma kwa
wakati na wenye tija.
Amebainisha
hayo wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi
wa Serikali za Mitaa (TALGWU) walipokutana Mjini Dodoma katika warsha ya
siku tano kuanzia Januari 29 hadi Februari 02, 2018 kujadili masuala ya
wafanyakazi nchini.
Waziri
Mhagama alieleza kuwa, kupitiswa kwa muswada ni moja ya utekelezaji wa
takwa la Ibara ya 11 kifungu kidogo cha kwanza cha Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ulipoona umuhimu wa kuweka mifumo ya hifadhi ili
Watanzania wapate manufaa hasa siku za uzeeni.
“Maamuzi
ya kuwa na Muswada huu umezingatia taratibu zote za kisheria ikiwemo
Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sera ya
Hifadhi ya Jamii, Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani unaoongoza katika
maswala ya Hifadhi ya Jamii”.Alisisitiza Mhagama
Muswada
huu umelenga kuunganisha mifuko ya Pensheni ambayo ni PSPF, LAPF, GEPF
NA PPF ili kukidhi kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi cha kuunganisha
mifuko hiyo ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuwa na mfumo
madhubuti utakaohakikisha mwanachama anapata mafao kwa wakati.
“Muswada
umebainisha kuwa jumla ya mafao 7 yatakayolipwa na mfuko huo itakuwa:
Fao la Pensheni, Warithi, Ulemavu, Uzazi, Ukosefu wa Ajira, Ugongwa na
Fao la kufiwa.” alifafanua Waziri Mhagama.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa TALGWU Bw. Tumaini Nyamhokya
aliipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kueleza kuwa ni wakati mwafaka
kwa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa kuunga mkono juhudi za
Serikali ikiwemo kuunganishwa kwa mifuko hii kwa manufaa ya wafanyakazi
wote wa umma.
“Niwaombe
watumishi wa umma wote kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha
maslahi ya watumishi na kwa asilimia 98 muswada huu umeyapitisha
mapendekezo na ushauri uliotolewa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
(TUCTA) na kuwekwa kwenye utekelezaji.”Alisema Nyamhokya.
Naye,
Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Suleiman Kikingo alisema kuwa kuunganishwa
kwa mifuko hiyo na kuwekwa kwa tozo ya asilimia tano kwa mfuko utakao
bainika kushelewesha mafao ya mwanachama itasaidia kupunguza changamoto
ya ucheleweshwaji wa mafao kwa wanachama.
No comments:
Post a Comment